SK ni kifupi cha jina la mwanzilishi na mmiliki wa blog hii, Suleiman Kidudu ambapo jina langu sahihi ni Suleiman Mohamed Kuleiman.

Kitaaluma Mimi ni Mtangazaji na Mwandishi wa Habari, najishughulisha katika kuandaa na Kutangaza Vipindi mbalimbali kuanzia Ngazi ya Habari, Siasa, Michezo, Burudani na Vipindi vya Mapenzi na Mahusiano. Kadhalika nimejikita katika Uandishi wa Habari na Makala za Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi, Burudani na Uandishi wa Simulizi za Mahuano ya Kimapenzi.

Suleiman ni mtoto wa kwanza Katika familia ya Watoto wa Tano wa Mzee Mohamed Seleman maarufu  (Mohamed Kidudu). Jina la Kidudu ni jina ambalo nimerithi kutoka kwa Mzee Mohamed Selemani ambae ni baba yangu mzazi.

Jina hili la kidudu lilitoka kwa Mzee Mohamed na kuhamia kwangu mara tu nilipofikisha miaka 10 kutokana na kipaji changu cha kusakata mpira wa miguu  wengi walinishangaa kwa kuwa umri wangu ulikuwa mdogo lakini mambo niliyokua nikiyafanya Uwanjani ndio yalipelekea wakanipachika Jina  la "Kidudu" likimaanisha kijana msumbufu mno na sikabiki niwapo Uwanjani.


Karibu SK News.