Na Muandishi wetu

Vyombo vya usalama nchini Nigeria vimesema vimewaokoa watu wawili waliotekwa nyara wakati wa shambulio dhidi ya msafara wa Marekani katika jimbo la Anambra kusini-mashariki mwa Nigeria siku ya Jumanne.

Msemaji wa polisi Ikenga Tochukwu hakutoa utambulisho wa wale ambao wameokolewa lakini alisema kuwa operesheni bado inaendelea na maelezo zaidi yatawasilishwa.

Watu saba walifariki katika shambulio hilo, huku Marekani ikisema hakuna rai wake aliyekuwa kwenye msafara huo, uliokuwa ukisafiri katika jimbo hilo lililokumbwa na ghasia na uasi wa kundi linalotaka kujitenga.