Na Mundishi wetu Kidawa

Mkutano wa 11 wa baraza la kumi la wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza jumatano ya tarehe 10 mei 2023 saa 3:00 asubuhi.

Katibu wa baraza la wawakilishi raya issa mlsellem ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika ofisi za baraza hilo huko chukwani Zanzibar.

Raya amefahamisha kuwa Mkutano huo utahusisha maswali na majibu ambapo afisi ya baraza la wawakilishi imepokea na kuratibu maswali 246.

Amesema baraza hilo pia litahusisha majadiliano ya bajeti ya serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema katika mikutano huo pia miswaada minne ya sheria itawasilishwa ikiwemo mswaada wa sheria wa fedha,

Mswada wa sheria ya kuidhinisha matumizi ya serikalikwa mwaka 2023/2024,

Mswada wa kufuta sheria ya kuzuia rushwa na kuhujumu uchumi Zanzibar namba  1 ya mwaka 2012 kutunga upya sheria sheria ya kuzuia rushwa na kuhujumu uchumi Zanzibar na mambo mengine yanayohusianana na hayo.