Na Muandishi wetu

Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) limetiliana saini Mkataba wa usimamizi na uendeshaji wa bandari ya Malindi na kampuni ya Africa Global Logistics kwa lengo la kuongeza ufanisi katika shughuli za uendeshaji wa bandari hiyo.

Kwa upande wa Serikali saini imetiwa na Mkurugenzi Mkuu wa ZPC, Nahat Mahfoudh huku kampuni hiyo ya nchini Ufaransa ikiwakilishwa na Tony Steaning.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dkt. Khalid Salum amesema mkataba huo haumaanishi bandari hiyo imebinafsishwa bali ni kwa ajili ya usimamizi hatua itakayoongeza ufanisi wa ushushaji na upakiaji wa mizigo katika meli.

Nae Mwakilishi wa kampuni ya Africa Global Logistic Tony Steaning ameahidi kufanya kazi kwa ufanisi ili kuimarisha utendaji wa bandari ya Malindi.