Na Muandishi wetu

     

    Katika hali isiyo ya kawaida Binti mmoja ( 13 ) amejifunguwa Mtoto huku Familia ya yake ikishikwa na mshangao kutokana Binti huyo kutokuonyesha dalili yoyote ya Ujauzito hapo kabla.

Tukio hilo limetokea tareh 3 March 2023 Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati mtoto  huyo alipokuwa akirudi Skuli alilalamika kuwa anaumwa na Tumbo na baada ya Muda mfupi akajifunguwa jambo ambalo liliwafanya wengi kupatwa na taharuki .

Nae mama mzazi wa Mtoto huyo amesema kuwa hakuona viashirio  vyovyote vya Mtoto wake na badala yake alikuwa akifanya shughulizake,  ikiwemo kwenda Shule .

Aidha Baba mzazi wa mtoto anaetuhumiwa kufanya tukio ilo Ndg Khamis Hussein Abdalla amezipokea taarifa hizo kwa simanzi kutokana na Umri wa Binti huyo.