Na Muandishi wetu  Donald Martin

 

Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imesema mkwamo uliokuwa ukitatiza mchakato wa ufilisi wa iliyokuwa benki ya FBME Tanzania tawi la Cyprus umetatuliwa.

Mkurugenzi wa DIB, Isack Kihwili amesema Disemba 12, 2022 Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia DIB ilifikia makubaliano na benki kuu ya Cyprus kuhusiana na ufilisi wa tawi la FBME Cyprus.

Amesema baada ya changamoto ndogo ndogo za kisheria kuwekwa sawa ufilisi wa tawi la Cyprus utaanza rasmi na baada ya hapo waliokuwa wateja wa benki hiyo watalipwa stahiki zao.