Na Muandishi wetu

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Hemed Suleiman amesema viongozi wakuu wa Serikali wamekuwa wakijumuika  na wananchi katika matukio mbalimbali ili kuwa karibu nao waweze kueleza changamoto zinazowakabili ziweze kutatuliwa.

Akiwasilimia waumini wa msikiti wa Biziredi Mkoa wa Mjini Magharibi alipojumuika nao katika ibada ya sala ya Ijumaa.

Amesema azma ya serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii na fursa mbalimbali za kiuchumi.

Aidha Alhaj Hemed amewasisitiza wananchi kushirikiana na Serikali katika kuimarisha amani na utulivu ili kuweza kufikia maendeleo yanayotegemewa.

Akitoa khutba katika sala hiyo, Sheikh Tahir Ali Said amewasisitiza waumini wa dini ya kiislamu kuwa na utamaduni wa kutoa sadaka katika maisha yao ya kila siku amesema kutoa sadaka ni miongoni mwa matendo yatakayomsaidia muumini kukingwa na moto.