Na Muandishi wetu

Kamishna wa polisi Zanzibar CP Hamad Khamis ameahidi kuwahimiza askari wa jeshi hilo kuendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi na za jeshi la polisi ili wasifunje haki za binadamu.

Ametoa ahadi hiyo katika mafunzo yaliyotolewa na Tume ya haki za binadamu kutoa mafunzo ya haki za binadamu kwa maafisa wa polisi wa makao makuu ya Polisi Zanzibar.

CP Hamad amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa watendaji wa jeshi hilo na kwamna watatumia wakaguzi wa sheria kutoa elimu kwa wananchi kwa vile wengi wao hawazijui haki zao.

Nae Kamishna wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora Tanzania, Khatib Mwinyi amesema Tume hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuimarisha utendaji unaozingatia haki na utawala bora.