Na muandishi wetu

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka amesema jumla ya baa na kumbi za starehe 89 zimefungiwa baada ya kubaini kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya NEMC kwa kushirikiana na jeshi la polisi kufanya msako katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza na Dodoma kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga muziki kwa sauti ya juu ambayo ni kinyume cha sheria ya mazingira ya mwaka 2014.

Dkt. Gwamaka amesema wamezifungia baa na kumbi hizo za starehe kwakuwa sio mara ya kwanza kutenda makosa hayo licha ya kuonywa pamoja na kutozwa faini na NEMC.

Baa na kumbi za starehe zilizofungiwa ni 19 kutokea Kinondoni, 25 Ilala, 22 za Kigamboni na Temeke 12, Jijini Dodoma tano na 48Mwanza sita.