Na wandishi wetu

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya daladala waliokuwa wamepanda kugonga treni katika makutano ya barabara na reli eneo la kamata jijini Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 12 asubuhi wakati daladala hiyo inayofanya safari zake kati ya Machinga Complex na Kigamboni kugonga treni katika eneo hilo.

Kamanda wa kikosi cha reli Tanzania, Sebastian Mbuta amesema chanzo cha ajali ni dereva wa daladala kukaidi amri ya mshika kibendera aliyekuwa akisimamisha magari ya pande zote mbili ili kuruhusu treni hiyo kupita akidhani angewahi kupita lakini matokeo yake aliigonga treni.

Mbuta amesema majeruhi alikimbizwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hali zao zinaendelea vizuri ambapo baadhi yao walipata michubuko midogo.