Na muandishi wetu

Wizara ya Uchumi wa Bluu Zanzibar, imekabidhi Boti 32 za Uvuvi kwa Wavuvi na Wakulima wa Mwani pamoja na Mabwawa ya kisasa kwa Wafugaji wa Mazao ya Bahari Kisiwani Pemba

 Akizungumza na Wajasiriamali, katika hafla ya ugawaji wa Vifaa hivyo, katika Afisi za Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Pemba, Waziri wa Wizara hiyo, Mh. Suleiman Masoud Makame, Amesema Serikali imekusudia kunyanyua Wananchi wake kiuchumi hivyo amewataka Wajasiriamali, kuzitumia Boti hizo ili kufikia malengo pamoja na  kuendelea kuitunza Bahari..  

Mkurugenzi Mipango, Sera, na Utafiti, Wizara ya Uchumi wa Bluu Zanzibar, Sheha Idrisa Hamdan na Mkuu wa Wilaya ya Wete, Nd. Hamad Omar Bakar, wamesema ni imani ya Serikali baada ya kutolewa Vifaa hivyo kipato cha Wananchi kitaongezeka..

Vifa hivyo vilivyokabidhiwa vimegharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 1 kutoka katika Mfuko wa Ahuweni 19, kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Benk ya CRBK..