Namwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe:
Rashidi Hadidi Rashidi amewataka Wananchi wa Mkoa wa Kusini kuendelea kudumisha
Muungano wa Tanganyika na Zanizibar ili kulinda amani na mshikamano uliopo Nchini.
Akizungumza katika kilele cha
kuadhiimisha Muunganono ,huko katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
(SUZA) Tunguu, amesema Muungano huo ulio dumu kwa Miaka 59,umekua
chachu ya kuleta maendeleo katika Taifa ikiwemo Afya, elimu, maji safi na
salama na miundombinu ya barabara.
Amesema hata hivyo katika kuadhimisha
miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Wananchi wa Mkoa huo wanakila
sababu ya kutathmini misingi iliyoachwa na Waasisi wa Muungano ili iendelee
kuimarisha umoja,amani na utulivu wa taifa letu.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kusini Rajab Yussuf Mkasaba ameahidi kupitia Wananchi
wa Wilaya ya Kati na Kusini kuenzi na kuulinda Muungano kwa ajili ya
kuleta maendeleo
Akitoa neno la shukurani kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa Ndg: Makame Ramadhan
Makame amesema kupitia kauli mbiu ya Muungano huo Chama cha Mapinduzi
kitaendelea kutoa Elimu ya kuutunza pamoja na kuwaenzi waasisi wa
muungano.
Itakumbukwa kuwa kila ifikapo
tarehe 26/4 serikali huadhimisha sherehe hizo kitaifa ambapo kwa mwaka huu
sherehe hizo zimefanyika kimkoa ambapo kauli mbiu ni “umoja na
mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu”.
0 Maoni