Na muandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala
Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amesema ipo haja ya kuendelea kuielimisha jamii
hususan vijana ili waweze kuijua vyema historia ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ili kuepusha upotoshwaji wa historia hiyo.
Ametoa kauli hiyo wakati akizindua kongamano la kuadhimisha
miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha
Zanzibar (ZU) Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,
Amesema hatua hiyo itawaongezea uelewa pamoja na kuyajua mafanikio
yaliopatikana kutokana na ushirikiano mzuri baina ya pande mbili za Muungano.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi Rashid amesema
kongamano hilo limekuja ili kuwapa elimu vijana kutokana na kuwa vijana wengi
hawajui historia ya muungano.
Kwa upande wake, Muhadhiri muandamizi chou cha Uandishi wa
Habari Zanzibar, Ali Shaaban Juma amewataka wasomi kufanya tafiti na kuandika
kwa kina juu ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika ili kuwa na historia yenye taarifa sahihi.
Nao baadhi ya Vijana walioshiri katika kongamano hilo wameahidi
kwenda kuwaelimisha vijana wenzao juu ya elimu waliyoipata kwenye kongamano
hilo.
Kongamano hilo la siku moja lililowashirikisha viongozi wa chama
cha mapinduzi wa Mkoa wa Kusini unguja , mabaraza ya vijana pamoja na wanafunzi wa
vyuo vikuu ambapo mada ya kuhusu historia na faida ya Muungano.
0 Maoni