Na muandishi wetu
Waumini wa Dinini ya
Kiislamu na Madhehebu mengine kutoka Mkoa wa Kusini Unguja wameunganakwa pamoja katika dua na sala ya kuliombea taifa
la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ili nchi izidi kuendelea kuwa na amani na
utulivu.
Dua hiyo iliyofanyika
katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Tunguu wilaya ya Kati
ni miongoni mwa muendelezo wa maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar.
Akizungumza na waumini
hao Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Rajab Yussuf Mkasaba, amesema kufanyika kwa
dua hiyo ni moja ya ibada itakayosaidia kuwengeza nuru na mshikamano katika
kuenzi na kuudumisha muungano.
Amesema nchi
mbalimbali ziliungana na kushindwa kufikia malengo hivyo kuendelea kwa muungano
ni moja ya jitihada zinazoendelea kufanywa na viongozi wanayoiyongoza nchi
katika kudumisha muungano huo.
Hivyo alitumia fursa
hiyo kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana katika mambo mema na kukatazana
maovu ili nchi izidi kupiga hatua kimaendeleo.
Wakiongoza dua hiyo ya
pamoja Kadhi wa Wilaya ya Kusini Unguja
Abdul azizi Salehe Juma na viongozi wa Kanisa la Katoliki na Kanisa la
Anglikana waliomba dua kwa Mwenyezi Mungu kuendelea kuutia nguvu muungano
sambamba na
kuwaomba waumini
kuzidi kuendelea kuwaombea dua waasisi wa muungano na viongozi waliopo
madarakani ili wazidi kuuenzi muungano kwa faida ya vizazi vya badae.
0 Maoni