Na mwandishi wetu Maulid Khamis Pemba.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Muungano Mh. Hamad Hassan Chande, amesema yuko tayari kutoa ushirikiano katika vituo vya afya katika kuhakikisha jamii inapatiwa huduma bora kulingana na utaalamu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya tiba.

 Mh. Chande ameyasema hayo, huko katika Hospitali  ya Wete wakati alipokuwa akizungumza na madaktari wa vitengo tofauti vya Hospital hiyo, ambapo amesema tayari ameshaomba ufadhili ambao utasaidia upatikanaji wa vifaa vya matibabu kwa watoto njiti pamoja na vipimo vyengine kwendana na wakati.

Nao baadhi ya Madaktari wa Hospitali hiyo wametoa shukurani zao kwa Mbunge huyo,kwa kuwa na moyo wa kuunga mkono upatikanaji wa huduma bora kwa watoa huduma pamoja na jamii.