NA MAULID KHAMIS, PEMBA.

Wakulima wa Mwani shehiya ya kukuu ,Wilaya ya Mkoani wamepatiwa mafunzo ya kuchakata Mwani, ili kuongeza thamani ya zao hilo kuweza kukidhi soko la ndani na nje ya Nchi.

Akitoa mafunzo hayo, Afisa kutoka kitengo cha mwani Pemba, Hidaya Khamis Hamad, amewataka wakulima hao kuyatumia vyema mafunzo wanayopatiwa kwa lengo la kuongeza thamani utakao changia kukuza pato la mtu moja mmoja na Taifa kwa ujumla.

 Afisa ukaguzi na udhibidi ubora wa bidhaa kutoka taasisi ya viwango Zanzibar, Hamad Juma Khatib, amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kutengeneza bidhaa zenye ubora na kuhakikisha zinapata usajili kutoka katika Taasisi ya ZFDA.

 Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kwakuwapatia mafunzo hayo yenye lengo la kuongeza thamani ya zao la mwani.

Mafunzi yaliyotolewa katika hafla hiyo ni utengenezaji wa Sabuni na mafuta kutumia Mwani unaozalishwa kwa wingi na wakulima hao.