RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Viongozi mbalimbali wa Serikali  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchi Uganda leo 8-10-2022, kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 ya Uhuru wa Uganda, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Na Mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesafiri kuelekea nchini Uganda katika kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 Ya Uhuru.

 Rais Mwinyi anakwenda nchini Uganda kuhudhuria sherehe hizo akimuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu

 Rais Mwinyi katika safari hiyo ameongozana na Mke wake mama Mariam Mwinyi ambapo viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimia na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Nchini Uganda kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 ya Uhuru wa Uganda, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan