Na mwandishi wetu
Wananchi wametakiwa
kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na serikali ili katika kuleta maendeleo
ili kuweza kufikai malengo iliyojiwekea.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo alipojumuika na
Waumini katika swala ya Ijumaa katika Masjid Jamii Taqwa Dunga Skuli Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema ni
wajibu wa kila mwananchi kuunga mkono jitihada zinzochukuliwa na serikali kwa
wananchi wake ili kuwaondolea usumbufu wa upatikanaji wa huduma muhimu za
kijamii.
Mhe. Hemed amewataka
wananchi kutosita kutoa taarifa pale wanapoona kuna uharibifu wowote wa
miundombinu na uvunjifu wa amani katika maeneo yao ili serikali iweze kuchukua
hatua za kisheria kwa maslahi ya wazanzibari.
Aidha Alhajj Hemed
amewataka waumini na wananchi kuwaenzi watu wenye mahitaji maalum wakiwemo
wajane,walemavu na mayatima ili kuwawekwa sawa na binadamu wengine katika
kupata mahitaji na mapenzi miongoni mwao.
Amesema kuwa kila
mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anatoa ushirikano wa hali ya juu
kwa makundi hayo maalum ili kuondosha changamoto ambazo huwakumba watu wa aina
hio ikiwemo suala la udhalilishaji.
Kwa upande wake Imamu
wa Msikiti huo Sheh. IS-HAKA VUAI KIDAWA amewataka
Waumini na Viongozi wanaosimamia mirathi kwa mayatima na wajane kusimamia haki
zao kama dini inavyosema ili kupata fadhila hapa duniani na kesho ahera.
Amesema ni wajibu kwa
kila muumini na kiongozi wa familia kuwa na malezi mazuri kwa mayatima na
wajane ili kuweza kupata fadhila za Allah S.W na kuwataka wazanzibari kurudisha
malezi ya zamani kwa vijana ili kupata jamii iliyo bora.
0 Maoni