Na mwandishi wetu
Serikali imeitaka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Saalam
(DIT) kuhakikisha kuwa inaongeza ufundishaji kwenye ujuzi wa bidhaa za ngozi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda
ameyasema hayo tarehe wakati alipotembelea chuo hicho kampasi ya Mwanza ili
kujionea maendeleo ya taasisi hiyo ikiwemo mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Umahiri
cha Teknolojia ya Ngozi unaoendelea chini ya Kampuni ya Comfix Engineering.
Amesema kuwa Serikali imetenga Shillingi Bilioni 19.6 kwa
ajili ya ukarabati wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Saalam (DIT) Kampasi ya
Mwanza utakaoleta mapinduzi ya elimu kwa vitendo katika teknolojia ya ngozi
nchini.
Prof. Mkenda amesema serikali inafanya ukarabati huo katika
mpango wake wa kuhakikisha DIT inakuwa kitovu cha utoaji mafunzo ya ufundi wa
utekengenezaji bidhaa za ngozi ikiwa ni pamoja na viatu, mikanda, waleti,
mabegi na mipira jambo ambalo litasaidia kutengeneza ajira kwa vijana wengi
kanda wa ziwa na Tanzania kwa ujumula.
Awali Mwenyekiti wa baraza la DIT Mhandisi Dkt. Richard
Masika akimkaribisha waziri wa elimu katika taasisi hiyo amesema DIT imekuwa
ikitoa mafunzo ya ufundi wa utengenezaji bidhaa za ngozi kwa nadharia na
vitendo ili kuwajengea uwezo vijana wa waweze kushindana katika soko la ajira
kitaifa na kimatafa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ameanza ziara ya siku nane katika mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita na Kagera.
0 Maoni