Mkuu wa Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja Marina Joel Thomas

Na mwandishi wetu

Masheha wa Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja,  wameshauriwa  kuihamasisha jamii kujikita Zaidi  katika ukulima wa kilimo  cha  miwa  ili  kuongeza kipato na kukidhi  uzalishaji wa mali ghafi ya  kiwanda  cha Sukari Mahonda

Mkuu wa Wilaya hiyo Marina Joel Thomas, amesema hayo alipokuwa katika kikao na Masheha wa Wilaya hiyo na Uongozi wa kiwanda cha sukari Mahonda waliofika katika ofisi ya Baraza la Mji Kati Dunga kwa lengo la kuwashajihisha wananchi kulima kilimo hicho.

Amesema licha ya juhudi mbali mbali  zinazoendelea kuchukuliwa  na uongozi wa kiwanda  hicho kuzalisha zao hilo lakini  bado wanakabiliwa  na uhaba wa maeneo ya uzalishaji  wa zao hilo  hivyo  kupatikana kwa maeneo mengine kutasaidia kuongezeka kasi ya uzalishaji wa  sukari kwa wingi  hali itayochochea  ukuwaji wa uchumi  wa nchi na wananchi kwa ujumla.

Nao baadhi ya viongozi wanaosimamia  uendeshaji wa kiwanada  hicho Bwana  Mohamed Said Dimwa na Bwana Hindi Said Mohammed wamesema ikiwa masheha watahamasisha ipasavyo wananchi katika maeneo yao itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kupata ajira kwenye sekta hiyo..

Nao baadhi ya masheha wamepongeza hatua ya uongozi wa kiwanda hicho na kuahidi kuihamasisha jamii juu  ya suala hilo ambalo litawaletea manufaa katika maisha yao ya kila siku.

MAJINA YA MASHEHA HAO : ND:Tatu Sheria Shaban Sheha wa Shehia ya Cheju Zawiani na Sheha waShehia ya Jumbi Muhidini Haji Machano waliahidi.