Na Mwandishi nwetu
Makamo wa Pili
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Adbullah anatarajiwa
kuwa Mgeni Rasmi katika Michuano ya Green Cup hatua ya Nusu Fainal
inayotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ya Desember 5, 2021, katika Uwanja wa
amani
Kasmir Haji
ambae ni katibu msaidizi Mkuu Idara ya Uhamasishaji na Chipkizi Tanzania ambae
anaefanyia kazi zake Zanzibar, ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari
katika kikao kilichofanyika hii leo Dec 2, 2021, kwenye ukumbi wa Ofisi za umoja wa Vijana (UVCCM)
Zanzibar, zilizoko Gymkana Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharib.
Amesema Hatua
hiyo ya Nusu fainali itakayohudhuriwa na Mhe Hemed itakuwa na michezo Miwili
ambayo yote itachezwa siku moja, ambapo kutakuwa na Mchezo wa Mapema saa nane
utakaowakutanisha Mkoa wa Pwani na
Tabora na Mchezo utakaofuatia utachezwa saa kumi kwa kuwakutanisha Wenyeji
Magharibi wawakilishi pekee wa Zanzibar ambao watacheza na Mkoa wa Morogoro
Katibu Kashmiri
amesema Mkoa wa Morogoro,Tabora, Pwani na Mkoa wa Mgharibi ndio ambao
wamefanikiwa kupita katika hatua hiyo Nusu fainal na Maandalizi kuelekea mchezo
huo tayari yameshakamilika.
‘‘Maandalizi
yote yamekamilika na mhezo wa saa nane tutakua nae Katibu Mkuu wa Umoja wa
Vijana Tanzania ndie atakaekua Mgeni Rasmi na mchezo wa saa kumi tutakua na
kiongozi Mkubwa ambae ni makamo wa Pili wa Rais Zanzibar na Jumamosi
tunatarajia kupokea timu zote zinazokuja kutokea Tanzania Bara’’.
Kwaupande
Mwengine Katibu Kasmiri amesema kutazama michezo hiyo ni bure na hakuta kuwa na
kiingilio chochote hivyo, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwawingi
kushuhudia burudani mabli mbali siku hiyo ikiwemo Benin na n.k
0 Maoni