Bi Hidaya Juma Hamad, Mfamasia kutoka Wakala Wa Chakula, Dawa na Vipodozi(ZFDA) akizungumza na Waandishi ambao pichani hawapo

Na Suleiman Mohamed

Wakala wa udhibiti Chakula,Dawa na Vipodozi  Zanzibar (ZFDA) wamesema wamejiridhisha kupitia miongozo ya Shirika la Afya Duniani kua  Chanjo za UVICO 19 zilizothibitishwa na Serikali kutumika Zanzibar ni salama na zina ubora unaokubalika.

Hayo yameelezwa na ----Bi Hidaya Juma Hamad, Mfamasia kutoka Wakala Wa Chakula, Dawa na Vipodozi,  wakati  wa Mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa Habari juu ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo yaliyofanyika katika Hotel ya Golden Tulip Bububu Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

 Amesema Wakala wa Chakula Zanzibar kabla ya kuingia kwa Chanjo hapa Nchini walitumia kila Njia kuhakikisha wanajiridhisha Ubora na usalama wa Chanjo hizo kama ilivyo kwa Chanjo nyengine kuhakikisha zinakua salama na ubora unaokubalika

‘‘tulishirikiana na Shirika la Afya Duniani  katika kutumia Miongozi katika kujilijiridhisha kua inakua na Ubora na Usalama pia hua tunafanya mawasiliano na wenzetu mara kwa mara kwa pale ambapo tunapohisi iko haya ya kujiridhisha zaidi na sio kwa chanjo hii ya UVICO 19 tu hata chanjo nyengine zinazoingia hapa nchini hua tunajiridhisha kabla ya matumizi’’

Kwa upande wake Mratibu wa Kitengo cha Elimu ya Afya, kutoka Wizara ya Afya, Wazee, Ustawi wa Jamii Wanawake na Watoto Zanzibar Bi Halima  Khamis amesema Serikali inatoa chanjo hizo bure kwa lengo la kuwakinga wananchi wake na UVICO 19 hivyo wananchi waepukane na dhana potofu na badala yake wajitokeze kwa wingi kupata Chanjo hiyo.

Amesema katika kuhakikisha hudma za Chanjo zinawafikiwa wananchi wengi Serikali imeongeza Vituo vya kutolea huduma katika kila Wilaya na Mikoa kwa Unguja na Pemba ambpo kuna jumla ya Vituo vipatavyo Thelathini na Nane (38).

Hadi sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Tayari imeidhinisha Jumla ya Chanjo sita kutumika hapa Zanzibar ikiwemo Sputnilc Light, Sinovac, Moderna, Pfizer,sinophac, na Johnson & Johson.

Mratibu wa Kitengo cha Elimu ya Afya, kutoka Wizara ya Afya, Wazee, Ustawi wa Jamii Wanawake na Watoto Zanzibar Bi Halima  Khamis, akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari ambao hawaonekani pichani
wakifunzi kutoka  Wizara ya Afya, Wazee, Ustawi wa Jamii Wanawake na Watoto Zanzibar
Washiriki wa mafunzo ambao ni waandishi wa Habari kushoto wakisikiliza wasilisho la mada linalotolewa ufafanuzi na Moja ya watoa mafunzo hayo