Na mwandishi wetu

Chama Cha Democrasia Makini ofisi ya Zanzibar Kuiunga mkono asilimia Mia Moja (100) hutuba ya Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi alioitoa hapo juzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege  Mkoa wa Mjini Mgharib. 

 Katika Taarifa hiyo aliyohutubia kwa vyombo vya Habari akiwa Ofisini kwakwe Taveta Wilaya ya Mjini, Katibu katibu Mkuu wa Chama hicho Ameir Hassan Ameir amesema hutuba hiyo ya Dr Mwinyi imeleta matumaini makubwa kwa wananchi wa Zanzibar.

 Amesema hotuba hiyo imeainisha namna Serikali ya Dr Mwinyi watakavyoshuhulika na Changamoto zinazowakabili wananchi hasa katika sekta ya Elimu, Afya, Maji, Umeme na kuwawezesha wajasiriamali maeneo ambayo naamini yakifanyiwa kazi vizuri yatachangia pakubwa kuinua uchumi wanchi.

 Aidha amewaomba wasaidizi wake ikiwemo Mawaziri, Makatibu na wataalum wa idara kuhakikisha wanafanya kazin kwa uaminifu na kuhakikisha wanamsaidia Mh Rais kutimiza azma yake kwaWananchi wa Zanzibar

 Katika hatua nyengine Amer Hasan Amer amemuomba Mh Rais kuhakikisha anasimamia vema  Fedha zilizotolewa na IMF ili zitumike ipasavyo katika kusaidia Changamoto za wananchi.