Na mwandishi wetu
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano wake na taasisi pamoja na mashirika yote
yenye nia kushirkiana na Serikali katika kuwaletea huduma wananchi wake.
Mhe. Hemed ameeleza
hayo wakati akizungumza na viongozi wa Shirika la Kimataifa la maendeleo
Duniani, linalosaidia kutoa huduma za kuwafikia watu wenye ulemavu Duniani
(CBM) waliofika Afisini kwake Vuga jijini Zanzibar.
Amesema Zanzibar kuna
uhitaji mkubwa wa huduma mbali mbali kwa wananchi wake, hivyo ujio wa Shirika
hilo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikia wananchi, na kuwapatia huduma
ikiwemo matibabu ya macho sambamba na kuwasaidia watu wenye ulemavu.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar ameeleza kuwa, Serikali haina pingamizi yoyote juu ya utekelezaji
wa huduma zinzotolewa na CBM, na ameuagiza uongozi wa Wiara ya Afya Ustawi wa
Jamii Wazee Jinsia na Watoto, kuhakikisha mpango huo unaanza haraka utekelezaji
wake kwa kutoa huduma kwa jamii.
Nae, Mkurugenzi mkaazi
wa shirika la CBM Nesia Mahange amesmea shirika lao limeamua kuunga mkono
jitihada za serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na uhitaji mkubwa uliopo wa
huduma za macho pamoja na masuala mbali mbali ya kijamii yanayohusu mambo ya
kimaendeleo.
Mkurugenzi Nesia ameleza kuwa shirika la CBM lina zaidi ya miaka Hamsini (50) tangu kuanzishwa kwake na linatoa huduma za rasilimali fedha,utaalamu, kujenga miundombinu, kutoa elimu jumuishi na kusomesha wataalamu kupitia sekta ya Afya ya macho, Elimu Jumuishi, Makaazi pamoja misaada ya huduma za kibinadamu itokanayo na masuala ya maafa.




0 Maoni