Na mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Afisi ya
Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga amesema Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kufanya jitihada mbali mbali katika kuboresha
vivutio vya uwekezaji hapa nchini.
Ameyasema hayo Afisi
kwakwe Mwanakwerekwe wakati alipokutana na Kaimu Kamishna kutoka Ubalozi wa
Uingereza Nchini Tanzani Bw. Rick Stern aliekuja kwa lengo la kuelezea kuhusu
mkutano wa majadiliano ya Kiserikali baina ya Serikali ya Tanzania na Uingereza
katika kongamano la biashara la uwekezaji, usimamizi wa kodi pamoja na
utaratibu wa kutunga sera na sheria, litakalofanyika tarehe 16 Novemba
mwaka huu katika ukumbi wa J.N.I.C.C Jijini Dar- es- salaam.
Waziri Soraga amesema
kupitia mkutano huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inamatumaini makubwa ya
kujadili na kuangalia namna gani nchi hizi mbili zinashirikiana katika mambo
mbali mbali, na kusema kuwa Zanzibar inatumia teknolojia ya mtandao katika
kutangaza vivutio vya uwekezaji.
Kwa upande wake Kaimu
Kamishna kutoka Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzani Bw. Rick Stern amesema
mkutano huo utajumuisha mijadala mbali mbali itakayostawisha mashirikiano baina
ya Tanzania na Uigereza.
Katika mkutano huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itawakilishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali ambao wataelezea hatua za Serikali ya Mapiduzi ya Zanzibar zinazochukuliwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji pamoja na kuelezea mikakati ya utekelezaji wa sera ya uchumi wa buluu.




0 Maoni