Rais Mwinyi ameyasema hayo Novomber 3 wakati akiweka jiwe la Msingi katika
Hoteli ya Riu Jambo iliyopo Nungwi, wakati wa Ziara yake katika shamra shamra
za kuadhimisha Mwaka mmoja tokea aapishwe kuwa Rais November 2 mwaka Jana
(2020)
Amesema ni Vema Miradi mikubwa inayojengwa karibu na Jamii ikiwemo mahotel
yakawanufaisha wananchi wanaozungukwa na Miradi hiyo katika kuleta maendeleo
kwapamoja.
Katika hatua nyengine Rais Mwinyi amesema wawekezaji wa miradi hiyo wanapaswa kushirikiana
na Jamii katika kuwasaidia changamoto zinazowakabili ikiwemo changamoto ya
elimu, afya, maji na mengineyo kwa kushirikiana na Serikali.
Rais Mwinyi alipata nafasi ya kuweka jiwe la msingi katika hoteli nyengine ya Emerald Zanzibar Resort and SPA iliyopo matemwe ambapo baada ya kuweka jiwe la msingi alipata nafasi ya kuwasalimia wananchi wa Matemwe Mbuyuni huku akiwataka kuendelea kuthamini sekta ya utalii kwakua ndio sekta inayochangia kukua kwa pato la Taifa.
Nao wawekezaji wa Hoteli ya Riu Jambo ambapo ujenzi wake ulianza Januarimwaka huu 2021 waliwahakikishia wavuvi wa maeneo hayo kwamba mradi wa Hoteli yao utakapokuwa tayari kufanya kazi samaki wote watakaovuliwa katika eneo hilo watanunuliwa na hoteli yao ili kuhakikisha wavuvi hao wanapata soko la uhakika pamoja na kuwajengea soko na miradi mengine ya jamii.
Kwa mujibu wa maelezo ya uongozi wa Hoteli hiyo, mradi huo unatarajiwa ujenzi wake kumaliza mnamo Septemba mwakani 2022, na utaajiri wafanyakazi 400 huku hoteli hiyo itakuwa na vyumba 468 ambapo ujenzi wake utagharibu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 70.
Kwa upande wa Hoteli ya Emerald Zanzibar Resort and SPA ambayo ujenzi wake ulianza Novemba mwaka jana 2020 unatarajiwa kumaliza mwakani 2022, mradi ambao kwa akuanzia utakuwa na vyumba 250 na hadi kumaliza katika awamu zijazoitakwua na vyumba 1000.




0 Maoni