Ndugu zangu Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Iringa na Ndugu Watanzania mnaofuatilia matangazo haya ya moja kwa moja ya taarifa ya Wiki ya Msemaji Mkuu wa Serikali, HABARI ZA MCHANA!!!
1. Mkoa wa Iringa.
Lakini nyote mtakumbuka kuanzia bajeti hii ya mwaka huu,Serikali ilianzisha tozo maalum kwa ajili ya kuharakisha baadhi ya mambo (Tozo katika miamala ya simu). Na kwa sababu jambo hili limefanyika kwa uwazi ningependa pia wananchi wa Iringa mjue tozo hizi zimewanufaishaje.
i.
Ukarabati
wa Uwanja wa
Ndege Iringa;
ii.
Ujenzi wa barabara
za lami
iii.
Mradi wa ujenzi Hospitali ya Wilaya ya
Kilolo.
iv.
Ukarabati wa Mradi wa Maji Isimani –
Kilolo.
v.
Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya
ya Iringa.
vi.
Ujenzi wa Jengo la Utawala la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Mufindi.
vii.
Ujenzi wa Jengo la Utawala la Makao
Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Iringa.
viii.
Ujenzi wa Chuo cha VETA – Pawaga na
ix.
Ujenzi wa Daraja
la Tosamaganga.
i.
Ukarabati wa
Uwanja wa Ndege wa Iringa (Nduli) – Kazi inatarajiwa kugharimu shilingi Bilioni
41 na Milioni 126. Fedha hizi zote zimeidhinishwa katika bajeti hii ya mwaka
huu.
Hadi sasa ujenzi wa mradi
huu umefikia asilimia 30, mkandarasi yupo nyuma ya muda kidogo lakini Serikali
inaendelea kumsimamia ili akamilishe mradi kwa wakati. Mradi huu umepangwa kukamilika
mwisho mwa mwezi Machi 2022.
ii.
Ukarabati wa
mradi wa maji wa Isimani – Kilolo. Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya
shilingi Bilioni 9 na Milioni 270, mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa shilingi
Bilioni 4 na Milioni 200 na kazi inaendelea. Natambua kuwa mradi huu pia upo
nyuma ya muda na Serikali inaendelea kutia msukumo ili mkandarasi aukamilishe
mwezi Juni 2022 kama ilivyopangwa. Tunatarajia mradi huu uongeze lita Milioni 7
kwa siku kwa wananchi wa Isimani na Kilolo na maji yatayozalishwa yatosheleze
mahitaji kwa miaka 15 ijayo.
iii.
Kwa upande wa
Barabara na Madaraja – kazi zinaendelea kuimarisha barabara za lami na
changarawe pamoja na kujenga madaraja katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huu.
Mifano michache;
·
Barabara ya
Kidabaga – Bomalang’ombe (km 18.3), ujenzi utagharimu shilingi Bilioni 8 na
Milioni 167 hadi kukamilika kwake Januari mwakani 2022. Mpaka sasa kazi hii
imefikia asilimia 75.
·
Barabara ya lami
ya Sawala – Mkonge – Iyegeya (km 30.3), ujenzi utagharimu shilingi Bilioni 7 na
Milioni 174 hadi kukamilika kwake Juni 2022. Mpaka sasa mradi huu umefikia
asilimia 50.
·
Tunajenga daraja
la Tosamaganga. Ujenzi huu utagharimu Shilingi Bilioni 1 na Milioni 398. Daraja
hili limejengwa kwa awamu tofauti, awamu ya kwanza na awamu ya pili (tumetumia
shilingi Bilioni 1 na Milioni 406) na sasa umeidhinishiwa shilingi Bilioni
1 na Milioni 398 na unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu.
·
Tumeanza kujenga
barabara ya mzunguko ya hapa Iringa (Iringa Bypass) inayoanzia kule
Igumbilo kuzunguka mlima hadi kutokea huku jirani na Uwanja wa Ndege wa Nduli
Kilometa 7.5. Tayari tumejenga nusu kilometa na kazi inaendelea kidogokidogo.
Lengo magari yanayokwenda Dodoma yasilazimike kuingia hapa Mjini na kusababisha
msongamano usio wa lazima.
·
Tumekamilisha
usanifu wa barabara ya Iringa – Msende kilometa 105 (kuelekea Hifadhi ya
Taifa ya Ruaha) na sasa mazungumzo yanaendelea na wadau wa maendeleo ili
tukijaaliwa mwezi Juni mwakani 2022 tutangaze zabuni na kupata mkandarasi
atakayejenga barabara hii.
Haya ni baadhi tu ya mambo yanayofanyika hapa Iringa,
kazi pia zinafanyika katika sekta ya uzalishaji mazao ya kilimo na mengine
ambayo siwezi kuyataja hapa kwa sababu ya muda.
Baada ya kuungalia Mkoa wa Iringa, naomba sasa nitoe
taarifa katika maeneo machache ya Kitaifa.
2. Ziara za Viongozi
Viongozi wetu Wakuu yaani Mhe. Rais, Makamu wa Rais na
Waziri Mkuu wameendelea kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje
ya nchi kwa lengo la kutembelea miradi ya maendeleo na kuzungumza na
Watanzania.
Hivi navyozungumza nanyi Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo Glasgow, Scotland ambako anahudhuria
mkutano wa 26 Umoja wa Mataifa (COP26) kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.
Mkutano huu unawakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali
130 kutoka Duniani kote na wanakutana kujadili athari ambazo dunia inazipata
kutokana na mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha ongezeko la joto duniani,
hewa ukaa na kuharibika kwa mazingira.
Inawezekana baadhi yetu tusielewa lugha hizi za
mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la hewa ukaa, lakini Tanzania nayo
inaathirika kutokana na madhara ya mabadiliko ya Tabia nchi.
Miongoni mwa athari tunazozipata ni pamoja na
kuongezeka kwa mvua kunakoleta athari katika uzalishaji, mazingira na makazi,
kuongezeka kwa kina cha maji katika Maziwa na bahari (wote tumeona kilichotokea
ziwa Victoria mwaka jana na kuzama kwa baadhi ya visiwa vyetu katika bahari ya
Hindi na maziwa), kuyeyuka kwa theruji katika Mlima wetu Kilimanjaro na mengine
mengi.
Sasa madhara ya athari hizi ni ya kidunia, huwezi ukajifungia nyumbani kwako na kupanga mipango
ya pekee yako kukabiliana nazo, zinahitajika juhudi za pamoja dunia, ndio maana
Wakubwa wa Dunia nzima wanakutana huko Glasgow, Scotland na Mhe. Rais wetu
ameona aende huko akatupiganie Watanzania.
Tayari kulikuwa na mikataba mbalimbali ya Kimataifa
ambayo nchi zimeridhia. Tanzania nasi tulisharidhia Mkataba wa Kyoto (mwaka
2002) ambao pamoja na mambo mengine unaagiza nchi 37 zinazozalisha hewa ukaa
nyingi kupunguza uchafuzi huo kwa asilimia 5, na Mkataba wa Paris ambao
tumeridhia mwaka 2018 unaotaka nchi zenyewe kuchukua hatua za kupunguza
uzalishaji wa hewa ukaa.
Ni katika mikutano huu, ndiko wakubwa hawa ambao nchi
zao zina maendeleo makubwa ya viwanda na ndio wanaozalisha hewa nyingi walikubaliana
nchi hizo zichangie Dola za Marekani Bilioni 100 kwa ajili ya kuwezesha
juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Fedha hizi ni kwa ajili ya kupelekwa katika nchi
mbalimbali kupitia taasisi zinafanya jitihada za kukabiliana na athari za
mabadiliko ya Tabia Nchi. Moja ya Taasisi hizo ni GCF (Global Climate Fund)
ambao wote mtakumbuka hivi karibuni imetoa fedha kwa benki ya CRDB kiasi cha
Dola za Marekani Milioni 100 (sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 230) kwa ajili
ya kuwakopesha Watanzania watakafanya shughuli za kilimo zinazosaidia katika
utunzaji wa mazingira.
Benki ya CRDB nayo imeongeza kiwango kama hicho hicho
kuongeza uwigo wa kutoa mikopo hiyo na sasa kuna kiasi cha takribani shilingi
Bilioni 460 ambazo zitawanufaisha wakulima takribani Milioni 6 hapa nchini.
Kwa hiyo kupitia dirisha hili kuanzia mapema mwakani
wakulima wataweza kupata mikopo itakayowawezesha kuongeza tija katika
uzalishaji kwa kulima eneo dogo na kupata mazao mengi, kutumia teknolojia za
kisasa katika kilimo zinazoepusha uharibifu wa ardhi, matumizi sahihi ya
viuatilifu, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, kurutubisha ardhi,
kuongeza kipato cha watu nakadhalika.
Sasa madirisha kama haya yapo mengi, na ni katika
Mkutano huu ambapo Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania anakwenda kukutana na Mwenyekiti wa taasisi hii ya GCF na
taasisi zingine zinazotoa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
LAKINI katika ziara hii pia Mhe. Rais Samia atakuwa na
mikutano mingine na atakutana na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa
Baraza la Biashara la Scotland ambao wanataka kuja kuwekeza hapa nchini
kwetu na atakutana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Boris
Johnson ambaye watazungumzia uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na
Uingereza.
Pia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amealikwa kuhudhuria
Mkutano wa Wakuu wa nchi 30 tu, kati ya wote 130 wanaohudhuria Mkutano huu na
atahutubia.
Kadhalika Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan atahudhuria
Mkutano wa viongozi wanawake (Women Leadership) ambao umeitishwa na First
Minister wa Scotland (ni kama Waziri Mkuu wa Scotland) na huko watazungumzia
ushiriki wa wanawake katika masuala ya mazingira na Mhe. Rais anatarajiwa
kuhutubia katika Mkutano huu.
Kwa upande wa Waziri Mkuu, leo yupo Dodoma ambako anaweka jiwe la msingi katika
sehemu ya mradi wa ujenzi wa nyumba 1,000 za kuishi watu katika maeneo ya
Chamwino na Iyumbu. Nyumba hizi zinajengwa katika juhudi za Serikali
kukabiliana na changamoto ya uhaba wa makazi katika Jiji la Dodoma hasa baada
ya Serikali kuhamia Dodoma.
Serikali iliamua kutoa mkopo wa shilingi Bilioni 20
kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya kuutumia kama mfuko maalum wa
mzunguko (Revolving Fund) kwa ajili ya kujenga nyumba na kuziuza ama
kupangisha.
Kwa hiyo katika kutekeleza mradi huu, ujenzi
unafanyika kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ujenzi wa nyumba 400 (100 zinajengwa
Chamwino na 300 zinajengwa Iyumbu) Awamu ya pili zitajengwa nyumba 375 na awamu
ya tatu zitajengwa nyumba 225.
Mhe. Waziri Mkuu ametoa wito kwa taasisi mbalimbali za
kifedha kuunga mkono juhudi hizi za kutatua changamoto ya makazi kwa Watanzania
wote sio tu kwa Jiji la Dodoma kwa kuwatumia NHC ama Watumishi Housing kujenga
nyumba za gharama nafuu ambazo Watanzania watamudu kuzinunua.
Na hapa Iringa, Mhe. Waziri Mkuu anatarajiwa kufanya ziara tarehe 13 Novemba, 2021
ambapo atafungua kongamano kuhusu mazao ya misitu litakalofanyika Mafinga na
kujumuisha wageni wa ndani na nje ya nchi.
3. Uwekezaji wa Serikali katika mashirika ya umma.
Kama wote mnavyojua, Serikali inamiliki mali katika
kupitia mashirika na taasisi mbalimbali ama kwa umiliki wa asilimia 100 ama kwa
ushirika na wabia. Serikali inasimamia mali hizi kupitia Ofisi ya Msajili wa
Hazina.
Hadi Juni 30, 2021 Ofisi ya Msajili wa Hazina ilikuwa
inasimamia mashirika ya umma 287 yanayojumuisha kampuni za biashara, taasisi 40
zinazomilikiwa na Serikali na kampuni za nje ya nchi kama 10 hivi.
Kwa ujumla hali ya uwekezaji wa Serikali katika
mashirika haya ni nzuri na mali ya Watanzania ipo salama na inaendelea
kukuongezeka thamani kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji na faida inayotokana
na gawio na makusanyo ya mapato yasiyo ya kikodi.
Takwimu za Ofisi ya Msajili wa Hazina zinaonesha kuwa
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita uwekezaji katika mashirika hayo
umeongeza thamani ya mali ya Serikali kutoka Shilingi Trilioni 64.45 hadi
kufikia shilingi Trilioni 67.06 (Hili ni ongezeka la asilimia 4).
Ongezeko hili kwa sehemu kubwa limetokana na kutekelezwa kwa sheria ya madini
namba 7 ya mwaka 2017 kifungu cha 10 na kanuni za madini za mwaka 2020 ambazo
zimetoa nafasi kwa Serikali kumiliki asilimia 16 ya hisa katika migodi ya
madini. Tayari tuna umiliki huo katika kampuni za North Mara Gold Mine Ltd, Bulyanhulu
Gold Mine ltd, Pangea Minerals Ltd, Twiga Minerals.
Sababu nyingine ni kuongezeka kwa ziada inayotokana na
kurejea kwa uthaminishaji wa mali pamoja na kukua kwa malimbikizo ya faida na
ziada ya taasisi na amshirika ya umma pamoja na umiliki wa hisa chache.
LAKINI PIA Ofisi ya Msajili wa Hazina pia hukusanya
mapato yasiyo ya kikodi, ambayo hukusanywa kutokana na michango ya asilimia 15
ya mapato ghafi ya taasisi na mashirika (kwa mujibu wa sheria ya fedha), kuna
mawasilisho ya asilimia 75 ya mapato yatokanayo na mtambo wa uhakiki wa
mawasiliano ya simu (TTMS) pamoja na asilimia 70 ya mapato ya ziada
inayozalishwa na taasisi na mashirika ya
umma.
Sasa mapato haya pamoja na mengine yasiyo ya kodi,
Ofisi ya Msajili wa Hazina imeendelea kuimarisha ukusanyaji ambapo katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita yamepanda kutoka shilingi Bilioni 425.47
za mwaka 2015/2016 hadi kuwa zaidi ya shilingi Bilioni 637.66. (Kuna
baadhi ya miaka yalifika mpaka zaidi ya shilingi Bilioni 885.64.)
Hata kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Sita kuna
dalili njema kabisa za usimamizi mali
hizi za Serikali kwani takwimu zinaonesha kati ya Aprili na Septemba mwaka huu
2021 shilingi Bilioni 299.14 zimekusanywa ikilinganishwa na mwaka jana kipindi
kama hiki ambapo makusanyo hayo yalikuwa shilingi Bilioni 227.32.
Inawezakana kuna baadhi yetu hatuelewi kuhusu umiliki
wa Serikali katika kampuni hizi na hapa nitatoa mifano michache
i.
Kiwanda cha
Sukari Kilombero, Serikali inamiliki hisa kwa asilimia 25. Na hivi
tunavyozungumza Serikali kwa kushirikiana na mbia wake tunafanya upanuzi wa
kiwanda hiki kwa kuwekeza shilingi Bilioni 571.6 ili kupanua uzalishaji kutoka
tani 127,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 271,000 katika kipindi cha miaka 3
ijayo.
ii.
Hapohapo
Kilombero, Serikali imeamua kununua shamba kuzalisha miwa la Mngeta kwa
asilimia 100. Na hivi navyozungumza shamba hili limekabidhiwa kwa Shirika la
Suma JKT kwa ajili ya kuendeleza uzalishaji na kuwasaidia wananchi.
iii.
Kiwanda cha
kuzalisha dawa cha Keko (Keko Pharmaceuticals Ltd). Serikali ilikuwa
inamiliki hisa kwa asilimia 40, lakini kutokana na kusuasua katika uzalishaji
mwaka 2019 iliamua kuongeza umiliki wake hadi kufikia asilimia 70.
Uwekezaji mkubwa umefanyika katika
kiwanda hiki kwa mwaka mmoja tu, ambacho kilikuwa kinazalisha dawa aina 1 na
sasa kinazalisha dawa aina 10. Uwezo wake wa kuzalisha vidonge umeongezeka
kutoka vidonge 1,500,000 kwa siku hadi kufikia vidonge 6,000,000 kwa siku.
Sasa hivi Keko Pharmaceuticals
Ltd inazalisha vidonge mbalimbali mbali kama vile Paracetamol, Metronidazole,
Erthromycin, Ampicilin, Pen V, Amoxicilin, Co-trimoxazole, Griseofulvin,
Ciprofloxacin na Diclofenac.
Uwezaji huu pamoja na kutusaidia kuongeza uhakika wa
upatikanaji wa dawa na kupunguza gharama za dawa pia kwa mwaka mmoja tu ambao
kiwanda hiki kimefanya uzalishaji baada ya uwekezaji wa shilingi Bilioni 7.5
kimezalisha faida ya shilingi Bilioni 1.4.
4. Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru
Kama nyote mnavyojua mwaka huu nchi yetu inatimiza
miaka 60 tangu ipate Uhuru wake. Tutatimiza miaka 60 tarehe 9 Desemba, 2021.
Hili sio tukio dogo na Serikali imeamua kutoa umuhimu
wa kipekee kwa tukio hili mwaka huu. Tunataka Watanzania wapate nafasi ya
kutosha ya kujua juhudi mbalimbali zilizofanywa na nchi yetu kwa miaka 60,
changamoto zilizojitokeza na jinsi tulivyokabiliana nazo mpaka leo.
Kutokana na hilo, kuanzia kesho shughuli za
maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru zitaanza. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenister
Mhagama atakuwa na mkutano na waandishi wa habari Jijini Dodoma katika
ukumbi wa PSSSF kuelezea namna shughuli za kuelekea maadhimisho haya
zitakavyofanyika.
Naomba kutoa wito kwa vyombo vya habari na waandishi
wa habari kufuatilia matukio haya yote, kurusha taarifa mbalimbali zitakazohusu
maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wetu.
Natambua kuwa vyombo vya habari vingi vimeanza
kutangaza masuala mbalimbali yanayohusu miaka 60 ya Uhuru, naomba na vyombo
vingine vijitokeze kufanya hivyo kwa sababu hili ni jambo la kizalendo kwa
ajili ya nchi yetu. Huu ni wakati wa kuionesha Dunia kwamba sisi Tanzania ni
Taifa imara, ni Taifa lililofanya udhubutu na likaweza kwa mambo mengi na
zaidi ya hapo ni Taifa ambalo pamoja na kujipigania lenyewe limetoa mchango
mkubwa Barani Afrika na kwingineko Dunia katika kupigania ukombozi, uhuru na
fikra.
5. Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA).
Ndugu zangu Waandishi wa Habari na Watanzania,
Serikali inatambua kuwa kuwa dunia ipo katika mapinduzi ya 4 ya viwanda, na
kama ilivyo kauli mbiu ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuwa “Tanzania lazima iende pamoja na Dunia” Nchi yetu imeamua
kuchukua hatua madhubuti ya kuwekeza katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) kwa kujenga mazingira ya shughuli na huduma mbalimbali kutolewa
kidigitali.
Moja ya hatua ambazo zimechukuwa ni kuwa na Wizara ya
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kuiwezesha kwa rasilimali nyingi
ili kufanikisha dhamira hii.
Katika mwaka huu wa Fedha Serikali iliamua kuongeza
bajeti ya maendeleo ya Wizara hii kutoka shilingi Bilioni 11 za mwaka jana
2020/21 hadi shilingi Bilioni 241.
Moja ya maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni katika
kupanua Mkongo wa Taifa na kuongeza uwezo wake. Kwenye Mkongo wa Taifa ambako
Serikali imewekeza zaidi ya shilingi Bilioni 677. Sasa kwa miaka yote Serikali
imekuwa ikitoa shilingi Bilioni 8 kwa mwaka kwa ajili ya kupanua Mkongo wa
Taifa lakini mwaka huu imeamua kuongeza fedha hadi shilingi Bilioni 170.
Lengo ni kuongeza kasi ya usambazaji wa mkongo na
kuongeza uwezo wake. Tangu mwaka 2009 tulipoanza kusambaza Mkongo wa Taifa
tumejenga kilometa 8,319 (kwa miaka 9), LAKINI kwa bajeti
tuliyoitenga mwaka huu tunakwenda kujenga kilometa 4,442 kwa mwaka mmoja.
Tunakwenda kuongeza uwezo wa mkongo mara nne ya uwezo uliopo sasa yaani kutoka
200G hadi 800G, hii itawezesha watoa huduma yaani hizi kampuni za simu
kuwasambazia huduma Watanzania wengi zaidi ya huduma zenye kasi zaidi.
Lakini pia tunapanua uwezo wa kuhudumia nchi majirani
ambazo zinatumia ama zinaweza kutumia Mkongo wetu, tumeshafikisha huduma Kenya,
Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Msumbiji na sasa tunajiandaa kwenda Congo DRC.
Kwa hiyo uwekezaji huu licha ya kwamba unatuimarisha
kutumia huduma za kidijitali lakini pia ni biashara kubwa ambayo nchi yetu
inaipata. Siku moja nitakuja kuwajulisha tunavuna mapesa kiasi gani kutokana na
uwekezaji huu mkubwa.
Lakini tukirudi kwenye dhamira yetu ya kujiimarisha
katika TEHAMA kama wote mtakumbuka Wiki iliyopita, Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iliadhimisha kongamano la 5 la Taifa la
TEHAMA lililofanyika katika Jiji la Arusha.
Kwenye kongamano hili Wataalamu wa TEHAMA takribani
845 walikutana na kampuni 27 zilifanya maonesho. Lengo likiwa ni kujadili
maendeleo ya TEHAMA katika nchi yetu, uwekezaji, usalama wa mtandao, kuangalia
ajira kwa vijana na mengine.
Kongamano hili limefanyika kwa mafanikio makubwa na
Wataalamu hawa wameweka maazimio kadhaa yakiwemo kuweka mazingira rafiki ya
kisera, sheria, tozo na kodi kwa vijana wanaojiajiri kupitia TEHAMA wakiwemo
wale wanaotengeneza mifumo mbalimbali ya biashara na huduma, kushirikisha
wadau, kuimarisha mifumo ya ufundishaji TEHAMA, kuhamasisha ujenzi wa viwanda
vya kuzalisha bidhaa za TEHAMA, kuvutia wawekezaji katika sekta hii na kujenga
mazingira ya kuvutia ukuaji wa biashara mtandao.
Sasa Serikali inafanya nini;
i.
Inahamasisha
wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika viwanda vya kuzalisha bidhaa za TEHAMA
kama vile simu, vishikwambi, computer na vinginevyo
ii.
Imeondoa kodi
kwa bidhaa hizo ili Watanzania wazipate kwa gharama nafuu.
iii.
Kupitia Wizara
ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Serikali imetenga
takribani shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Taaluma
ya TEHAMA (ICT Professional Center). Kituo hiki kitaanza kujengwa mwaka
huu pale Njedengwa Dodoma na matarajio yetu kikamilike Juni mwaka 2023 au kabla
ya hapo.
iv.
Mhe. Rais Samia
Suluhu Hassan ameahidi kuwa Serikali itajenga chuo kikubwa cha TEHAMA
hapa nchini. Chuo hiki kitakuwa kikubwa kuliko vyote katika ukanda huu
wa Afrika Mashariki na Kati.
Kwa haya yote lengo letu ni kuhakikisha Tanzania
inapika vijana kubobea katika masuala ya Tehama.
6. Mradi wa Kuendeleza Maliasili na Kukuza Utalii Kusini
mwa Tanzania (Resilient Natural Resources Management for Tourism and Growth –
REGROW).
Ndugu zangu Waandishi wa Habari na Watanzania, Sote
tunatambua kuwa moja ya maeneo yanayochangia fedha nyingi katika Pato la Taifa letu
ni Utalii. Utalii unachangia kwa asilimia 17.2 katika pato la Taifa, unaajiri
watu Milioni 1.6 na unachangia fedha za kigeni kwa asilimia 25.
Tanzania ni nchi ya pili Duniani kwa kuwa na vivutio
vingi vya utalii, ikitanguliwa na Brazil. Hata hivyo vivutio vyetu vimekuwa
havitunufaishi kwa kiwango kichastahili.
Yapo maeneo mengi ambayo kuna vivutio vingi vya utalii
lakini havitunuishio kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutufunguliwa kwa
miundombinu ya kuvifikia na kutokuwepo kwa huduma kwa Watalii.
Eneo la Kusini mwa Tanzania ni mojawapo ya maeneo
ambayo yanahitaji kufunguliwa kwa utalii. Ni kutokana na sababu hii Serikali
imeamua kuja na mradi huu uitwao REGROW.
Kupitia mradi huu Serikali imeamua kuimarisha
miundombinu na huduma za utalii katika hifadhi za Taifa za Ruaha, Nyerere,
Mikumi na Udzungwa ambayo yana kilometa za mraba 56,339. Utagusa mikoa ya
Iringa, Pwani, Mbeya, Dodoma, Njombe na Morogoro. Kuna vijiji 61
vitakavyonufaika katika Wilaya za Kilolo, Iringa Vijijini, Rufiji, Kisarawe,
Chamwino, Morogoro Vijijini, Mbarali, Kilombero, Kilosa, Mvomero.
Fedha zilizotengwa ni Shilingi Bilioni 345 kwa ajili
ya;
i.
Kujenga
miundombinu ya barabara kilometa 2,000, majengo zaidi ya 80, viwanja vya ndege
vya hifadhini 14. Usanifu wa miradi hii unaendelea.
ii.
Kununua magari
44 kwa ajili ya doria, usimamizi wa mradi, huduma za utalii nk. Magari haya
yameshanunuliwa.
iii.
Mitambo 16 ya
kutengenezea miundombinu ndani ya hifadhi imeshanunuliwa na imeanza kazi.
iv.
Kuna mkandarasi
yupo kazini katika skimu ya Madibila anaendelea na kazi ya kuboresha
miundombinu ya mradi huu.
v.
Mchakato wa
kuanza ujenzi wa kituo cha pamoja cha masuala ya utalii (One Stop Center)
umeanza. Jengo hili litajengwa pale Kihesa Kilolo kuanzia Juni mwakani 2022 kwa
gharama ya shilingi Bilioni 16 na Milioni 590.
Lengo hiki kiwe kituo cha
kisasa ambacho kitahudumia ukanda wote huu wa Kusini. Matarajio yetu hatua hizi
zitasaidia kuongeza idadi ya watalii na kuongeza pato la Taifa la nchi yetu.
7. Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano
dhidi ya Uviko 19.
Nyote mnafahamu kwamba nchi yetu inatakiwa itekeleze
miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.3 katika kipindi cha
miezi 9 tu.
Naomba kuwajulisha kuwa utekelezaji unaendelea, fedha
zimeshagawanywa kwenda katika sekta mbalimbali za utekelezaji ambako wananchi
katika maeneo husika wanatumia utaratibu Force Account yaani kupata
mkandarasi mmoja kwa haraka atakayetekeleza mradi badala ya utaratibu wa siku
zote wa kutangaza zabuni na ikapita mchakato wote.
Kwa wiki nzima iliyopita, mmeona jinsi Mawaziri
walivyotoa taarifa za namna mgawanyo wa fedha hizi ulivyofanyika na labda kwa
kujuisha ni kwamba Serikali imepeleka fedha hizi katika sekta mbalimbali kama
ifuatavyo;
i.
Tumepeleka
shilingi Bilioni 466.9 katika sekta ya afya
ii.
Shilingi Bilioni
367.6 katika sekta ya elimu
iii.
Shilingi Bilioni
302.7 katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
iv.
Shilingi Bilioni
231 kwa ajili ya Zanzibar (zimeshapelekwa)
v.
Shilingi Bilioni
139 katika sekta ya maji
vi.
Shilingi Bilioni
90.2 kwa ajili ya sekta ya utalii
vii.
Shilingi Bilioni
64.9 katika Wizara ya Elimu
viii.
Shilingi Bilioni
5.5 katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
ix.
Shilingi Bilioni
5 kwa ajili ya kuwawezesha vijana, wanawake na wenye ulemavu.
x.
Shilingi Bilioni
5 kwa ajili ya uratibu na utawala katika ngazi za Wizara, Mikoa na Serikali za
Mitaa.
Hivi ninavyozungumza nanyi kazi za ujenzi na michakato
ya ununuzi wa vitu mbalimbali imeanza. Kwenye maeneo yanayohitaji ujenzi,
wajenzi wameanza kupelekwa katika maeneo ya miradi baada ya kukamilisha
mazungumzo ya kuanza kwa ujenzi.
Mfano, fedha za ujenzi wa madarasa 15,000 zote
zimeshapelekwa kwenye akaunti za shule husika (kiasi cha Shilingi Bilioni
304) na tayari ujenzi katika baadhi ya maeneo umeanza.
Serikali inaendelea kuwakumbusha viongozi katika ngazi
mbalimbali kusimamia utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa kwa fedha hizi,
na wananchi kutosita kuhoji utekelezaji wake na kutoa taarifa kwa viongozi pale
watakapobaini vitendo vya kuhujumu miradi hii.
MUHIMU;
Watanzania tuna kila sababu ya kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Mhe. Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa juhudi kubwa
walizozifanya kupata fedha hizi.
Nataka kuwaambia ndugu zangu haikuwa Rais, wamepambana
sana hawa viongozi hadi wamefanikiwa, wamezungumza na wakubwa hawa wamepeleka
maandiko, wamekwenda kuyatetea mpaka tumefanikiwa.
Mimi nipo huku ndani naona, kama wangekuwa na mioyo
myepesi tusingepata. Na Fedha hizi zinakwenda kuleta mageuzi makubwa sana
kwenye huduma zetu za kijamii na katika uchumi.
8. Fedha za msaada.
Wiki hii nchi yetu imepata msaada wa shilingi
Bilioni 119 kutoka Serikali ya Ujerumani.
Fedha hizi zitaelekezwa katika masuala ya uhifadhi,
tutazitumia kununua magari kwa ajili ya kuwezesha shughuli za kukabiliana na
ujangili, kuweka mifumo ya kidigitali ya kufuatilia magari yanaingia
hifadhini pamoja wanyamapori wakubwa hasa walio hatarini kutoweka, kuwezesha
shughuli za utunzaji wa mazingira na kuboresha miundombinu ndani ya hifadhi
ikiwemo ujenzi wa mabwawa ya maji ya wanyama pamoja na kujenga viwanja vya
ndege vidogovidogo.
Halikadhalika zitatumika kuimarisha huduma za afya
hifadhini ikiwemo vituo vya upimaji wa Uviko-19 na huduma nyingine.
9. Mapambano ya Uviko-19.
Juhudi za kupambana na Uviko-19 zinaendelea. Wataalamu
wetu wanaendelea kutoa elimu kupitia majukwaa mbalimbali vikiwemo vyombo vya
habari, mitandao ya kijamii, kwenye maeneo yenye watu wengi n.k
Serikali inaendelea kutoa wito kwa Watanzania
kuendelea kuchukua tahadhari zote ambazo Wataalamu wanatuelekeza yaani kunawa
mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kuepuka misongamano isiyo ya
lazima, kuvaa barakoa, kula chakula cha lishe, kufanya mazoezi na kupokea
chanjo, kwa kuwa Uviko-19 au ugonjwa wa Korona bado upo, Watanzania wenzetu
bado wanapata maambukizi, wale ambao hawajachanjwa ndio wanaopatwa na ugonjwa
mkali na wengi wao ndio wanaopoteza maisha.
Utoaji wa chanjo unaendela nchi nzima, awali Serikali
ilileta dozi 1,058,400 aina ya JJ ama Jansen ambazo zimekwisha, na sasa
Watanzania wanaendelea kuchoma dozi aina ya Sinopharm kutoka nchini China
ambazo mtu anapaswa kuchoma dozi mbili. Chanjo aina ya Sinopharm zimekuja Dozi
1,065,600.
Kesho tutapokea dozi nyingine 500,000 aina ya
Sinopharm kutoka China, kuna zile dozi nyingine 500,000 za aina ya Pfizer
ambazo tuliahidi zingefika mwisho wa mwezi huu Oktoba, kulitokea changamoto
kidogo ya usafiri lakini wakati wowote hivi sasa zitaingia nchini.
Serikali inaendela kufanya juhudi nyingine za kupata
chanjo zingine ili Watanzania wengi zaidi wachome chanjo hizi na kujihakikishia
zaidi usalama dhidi ya Uviko-19.
Chanjo hizi zote zinaletwa nchini kwetu chini ya
mpango wa Shirika la Afya Dunia uitwao Covax Facility ambao unatoa bure chanjo
kwa idadi ya hadi asilimia 20 ya wananchi wa nchi husika, na hivyo hapa
Tanzania tunatarajia kupata dozi 11,800,000 kupitia dirisha hilo/mpango huo.
Hali ya Uchanjaji inakwenda vizuri, baada ya kuisha
dozi za chanjo aina ya JJ au Jansen sasa hivi uchanjaji unaendelea kwa chanjo
aina ya Sinopharm, takwimu za hadi Juzi tumeshatumia asilimia 5.5 ya chanjo
yaani watu 58,703 wamechanjwa tangu uchanjaji wa chanjo hizi ulipoanza tarehe
12 Oktoba, 2021.
Mikoa mitano inayofanya vizuri zaidi ni Mtwara, Mbeya,
Dodoma, Kagera na Ruvuma. Na inafuatiwa na Mikoa mingine 5 ya Arusha, Dar es
Salaam, Mwanza, Songwe na Pwani.
Serikali inatoa wito kwa wananchi ambao hawajapata
chanjo kujitokeza kupata chanjo hizi kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya
virus vya korona. Viongozi katika mikoa ambayo uchanjaji hauna kasi ya kutoshwa
wameagizwa kuongeza kasi ya uhamasishaji wananchi na kuhakikisha chanjo
zinapelekwa kwa wananchi katika maeneo walipo.
Lakini pia wananchi mnaopata chanjo aina ya Sinopharm
na mtakaopata chanjo aina ya Pfizer mnakumbushwa kuhakikisha mnarejea kupokea
dozi ya pili baada ya wiki tatu kama inavyoelekezwa na wataalamu. Na kwa
kutumia cheti ulichonacho kama haupo pale ulipochanjwa unaweza kwenda kwenye
kituo kingine chochote ukapate dozi ya pili ili ukamilishe kinga yako.
10.
Majibu ya maswali ya Wananchi na Waandishi wa Habari
wa Mwanza.
Sasa
Ndugu zangu Waandishi wa Habari wa hapa Iringa na Ndugu Watanzania, kama
nilivyosema majuma mawili yaliyopita nilikuwa Mkoani Mwanza ambako pamoja na
kutoa taarifa ya Wiki nilipokea maswali kutoka kwa Wananchi na Waandishi wa
Habari. Yapo niliyoyajibu palepale Mwanza nay apo ambayo nitayajibu leo kwa
sababu yalihitaji kufanyiwa kazi zaidi.
i.
Kuna Mwandishi wa Habari aliuliza kuhusu changamoto ya miundombinu ya barabara katika Jiji la mwanza inayosababisha msongamano wa magari hasa
katika barabara ya nyerere na kenyata.
Ni kweli Jiji la Mwanza
ambalo ni Jiji la pili kwa ukubwa hapa nchini likitanguliwa na Dar es Salaam
linakabiliwa na changamoto ya Msongamano mkubwa wa magari.
Kwa kutambua changamoto hiyo Serikali inachakua hatua
zifuatazo;
· Barabara ya Mwanza – Usagara, njia 4 inafanyiwa upembuzi yakinifu na
kazi hiyo itakamilika kufikia Mei 2022 ikiwa ni
maandalizi ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Upanuzi
wa barabara hiyo utaondoa msongamano katika barabara ya Kenyatta.
· Barabara ya Mwanza – Nyanguge, njia 4 inafanyiwa upembuzi yakinifu na
kazi hiyo itakamilika kufikia Disemba 2021. Upanuzi wa barabara hii utapunguza
msongamano katika barabara ya Nyerere.
· Ujenzi
wa Barabara ya Buhongwa - Kishiri kwa kiwango cha Lami inafanyiwa usanifu na utakapokamilika kazi ya ujenzi itaanza.
ii.
Kuna Mwandishi wa Habari ambaye alitaka kujua kuhusu kikokotoo, wafanyakazi hawajui hatima yao.
Majibu ni kwamba; Serikali inaendelea kutafakari suala hili lakini kwa
sasa malipo ya pensheni kwa Wastaafu yanaendelea kufanywa kwa utaratibu ule ule
wa zamani kama ambavyo kila mfuko wa hifadhi ya Jamii ulivyokuwa unawahudumia
wanachama wake. Kazi inayoendelea Serikali ikikamilika kwa kushirikiana na
vyama vya wafanyakazi mtajulishwa.
iii.
Kulikuwa na
swali la Mwandishi wa Habari wa Mwanza kuhusu msongamano wa magari yanayoingia
bandari ya Mwanza Kaskazini pale Jijini Mwanza.
Majibu ni kuwa; Hakuna
njia ya moja kwa moja ya kuingia bandarini (North Mwanza) njia kuu inayotegemewa
ni kupita katikati ya Kituo
cha Polisi.
Na eneo hili limewekewa zuio kwa sababu za kiusalama, maana
ikiruhusiwa maana yake tukiweka kituo cha polisi katika hatari ya uvamizi nan
yote mnajua vituo vya Polisi vina silaha zinazotumika kuwalinda raia na mali
zao. Wataalamu wa usalama wameona wakiruhusu njia hii kutumika kama ilivyokuwa
zamani upo uwezekano wa watu wenye nia ovu kuvamia kituo.
iv.
Kulikuwa na
swali la Mwandishi wa Habari wa Mwanza aliyetaka Serikali
iseme kweli kuhusu kadi za NIDA
(Vitambulisho vya Taifa), kwanini kuna ucheleweshaji wa kupata?
Majibu
ni kuwa; Serikali haifichi chochote kuhusu utoaji wa vitambulisho vya NIDA.
Mpaka
mwanzoni mwa Mwezi uliopita NIDA ilikuwa imesajili jumla ya watu 22,622,358
ambapo kati yake watu 19,036,378 walikuwa wamepatiwa namba za utambulisho.
NIDA
ilikuwa tayari imeshasambaza vitambulisho 8,567,407 katika Wilaya 117. Kati
yake kuna vitambulisho 1,322,649 vilikuwa vimepelekwa katika vituo lakini
wahusika walikuwa hawajafika kuchukua vitambulisho vyao.
Kwa
hiyo Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote ambao wamesajiliwa na hawapata
vitambulisho kwenda kwenye vituo walikoandikishwa wakafuatilie vitambulisho
vyao na kama kuna tatizo walieleze ili lifanyiwe kazi. Kumekuwa na changamoto
kwa baadhi ya watu ambao taarifa zao zimeonekana kuwa na dosari na hivyo NIDA
haiwezi kuendelea kuchapisha vitambulisho vya watu hao mpaka taarifa zao
ziwekwe sawa.
HATA
HIVYO; Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inaendelea na uzalishaji na ugawaji wa
Vitambulisho vya Taifa kwa mzunguko, utaratibu ulioanza Januari, 2021.
Kila mzunguko NIDA
inazalisha asilimia
25-30 ya maombi ya Wilaya husika ili kuwa na usawa wa uzalishaji na ugawaji wa
Vitambulisho nchi nzima.
Mpaka
sasa jumla
ya Wilaya 133 zimezalishiwa Vitambulisho kwa mzunguko wa kwanza.
Uzalishaji unaendelea
na vitambulisho
vinazalishwa na kupelekwa kwa Watendaji wa Mitaa na Vijiji.
Kwa upande wa Zanzibar
uzalishaji na ugawaji umefanyika kwa zaidi ya asilimia 90 katika Wilaya zote 11 na uzalishaji unaendelea.
Serikali
inatoa wito kwa waombaji wote wenye sifa za kupata
Vitambulisho vya Taifa na
ambao
hawajapata Vitambulisho kuwa
wavumilivu,
kwa kuwa watapatiwa vitambulisho kuendana na uhakiki unavyofanyika na ratiba
ya uzalishaji na usambazaji
iliyowekwa
v.
Kulikuwa na Swali la Mwandishi wa Habari wa Mwanza kwamba wafanyabiashara
wadogo wa Mwanza wameondolewa katika maeneo waliyopangiwa na hawana mahali
pengine pa kwenda.
Majibu ni kuwa; Ni kweli
wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) waliokuwa maeneo ya katikati ya Jiji la
Mwanza hasa eneo la Makoroboi wameondolewa LAKINI sio kweli kwamba
hawajapangiwa maeneo ya kwenda kufanya biashara.
Wamachinga walioondolewa
wamepangiwa maeneo ya Mchafukoga ambapo panaweza kuwaweka wafanyabiashara zaidi
ya 3,000. Wengine wamepangiwa Buhongwa (zaidi 3,000), Tambukaleli (zaidi ya
2,000), Soko la Igoma (takribani 1,000), eneo la Ukwaju-Igoma (nafasi ya
wamachinga zaidi ya 6,000), eneo la Soko la Mbao Igoma (nafasi ya Wamachinga
zaidi ya 500), eneo la Nyegezi karibu na Stendi ya mabasi inayojengwa (kuna
nafasi ya wamachinga kama 1,000).
Haya maeneo yote yamewekewa
huduma muhimu kama vile choo, maji, umeme. Katika eneo la Ukwaju hivi
navyozungumza viongozi wa Mkoa wa Mwanza wapo eneo la tukio wanahakikisha
huduma hizi muhimu zinawekwa ili wamachinga wakianza kupatumia wapate huduma.
Hata hivyo, Mwanza
kumejitokeza changamoto, kwamba sasa hata watu ambao hawakuwa Wamachinga lakini
kwa sababu wameona kuna ugawaji wa maeneo ya Machinga wamejitokeza kuomba
kupatiwa nafasi. Jiji la Mwanza linakadiriwa kuwa na Wamachinga 10,000 lakini
nafasi zilizopo ni zaidi ya idadi hiyo.
vi.
Kuna mwananchi aliuliza swali kuwa Watumishi wa umma wamepandishwa vyeo
na wana malimbikizo wanadai kwa miaka mitatu sasa hawajalipwa. Hayo
malimbikizo yatalipwa lini?
Majibu ni kuwa; Utaratibu wa kushughulikia madai ya malimbikizo ya mishahara
huanzia kwa mwajiri ambapo mtumishi mwenye madai ya malimbikizo hujaza fomu ya
madai ya malimbikizo na kuyawasilisha kwa mwajiri ambako hushughulikiwa na
kuikamilisha ipasavyo na kuiwasilisha Ofisi ya Rais -UTUMISHI.
Hata hivyo, kuanzia tarehe 24
Mei, 2021 umeanzishwa utaratibu ambapo fomu za madai ya malimbikizo ya
mishahara zinaingizwa na waajiri kupitia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na
Mishahara (HCMIS).
Kwa sasa uhakiki wa madai ya Watumishi 24,210 yenye thamani ya shilingi bilioni 86.5 yaliyowasilishwa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI unaendelea kufanyiwa kazi na ukikamilika watalipwa.




0 Maoni