Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Kaskazini Pemba Asya Sharif Omari amesema Raisi wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hasan ni Kiongozi Shupavu na aliejitolea kupigania maendeleo ya Watanzania
kwa kasi kubwa
Mbunge Asya
ameyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu akiwa Dodoma kwa lengo la kupata tathimni yake
kuhusu safari ya Rais Samia Nchini Misri, ambapo amesema Wanawake katika Nchi hii na Bara
zima la Afrika wanapaswa kujivunia kutokana na kuwakilishwa Vizuri na Uongozo
wa Rais Samia.
‘‘unajua wako ambao
hawakuamini kama mwanamke anaweza kua Rais na akafanya vizuri kiasi hki
anachofanya Samia yaani anatuwakilisha vizuri sana na sasa heshima ya mwanamke
imeendelea kuheshimiwa kutokana na kazi nzuri anayoifanya Mhe Rais Samia’’
Amesema ni vema watu
wakaelewa Safari ambazo Mhe Samia amekua akizifanya Nje ya Nchi zina tija kubwa
kwa Maslah ya Tanzania ikiwemo Nyanja za Utalii, mioundombinu,uwekezaji na
masuala mengine ya kulimo na Afya
‘ ‘Sikia mtangazaji
Rais Jana tu amerejea kutoka Misri na zafari yake haikua na usiri kila kitu
kilikua wazi, angalia ametembelea makampuni Makubwa ikiwemo wale wanaojenga
Bwawa la umeme, vilevile amefanya kikao na wafanyabiashara wa Misri katika
kuhakikisha fursa za uwekezaji zinatangazwa hapa nchini’’
Mbunge Amesema Raisi Samia katika safari yake Nchini
Misri ameshuhudia utiaji saini mkataba mmoja na hati saba za makubaliano kati
ya Tanzania na Misri ambazo hizo ameeleza kama hatua za kiamaendelea Serikali
iliyozifikia na suala la kukuza Diplomasia.
0 Maoni