MHE: Rashid Hadid Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
Na mwandishi wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Kusini imefanikiwa
kukusanya kiasi cha Shilingi Milion Sabiin na Saba na Tisini na Nane Mia Saba
na Nane (Tsh 7,798,708) kwa kipindi cha Miezi Mitatu ya Robo ya kwanza kuanzia Julai
hadi Sept mwaka huu.
Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji
ya kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi, katika kikao cha Baraza la Madiwani
lililofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo Kitogani Kusini Unguja, mjumbe wa Kamati hiyo Sharifa Omar Ali, amesema
Halmashauri ya Kusini awali ilipanga kukusanya Jumla ya Shilingi Milion
Sabiini na Sita lakini imefanikiwa kukusanya Milion Sabiin na Saba sawa na Asilimia
Mia na Moja hali ilopelekea kuvuka malengo waliojipangia.
Amesema hatua hio imefikiwa kutokana
na kuongezeka kwa vyanzo vipya vya mapato ikiwemo usafirishaji wa Mali Asili, Leseni
za Vileo na Maduka, Nyumba za kulaza wageni, minara pamoja na malipo ya faini
za uchafuzi wa mazingira na kuchelewa kukata Leseni.
Mapema Mkurugenzi wa Halmashauri
hiyo Ndugu Ali Rashid Suluhu amesema mbali na mafanikio yaliopatikana
katika ukusanyaji wa mapato lakini pia amewasisitiza makatibu wa kamati
ya kudumu za baraza hilo kuhakikisha wanafikisha kwa wakati taarifa za kamati
zao wanazo ziandaa ili kuiwezesha halmashauri kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la
Halmashauri ya Wilaya ya Kusini ndugu Mustafa Mohd Haji amewataka watendaji wa
halmashauri hiyo kuendelea kutimiza wajibu wao hasa katika suala zima la
kuongeza vyanzo vya ukusaji wa mapato kwa lengo la kuleta maendeleo kwa Jamii
na Serikali kwa ujumla.
Kikao hicho cha baraza la Halmashauri
kilichohudhuriwa na watendaji wa Chama na Serikali mbali ya kupokea ripoti
mbali mbali za utekelezaji wa utendaji kazi wa Baraza hilo pia imeridhia na
kupitisha vifungu vya matumizi ya Fedha Shilingi Milion Mia Moja na Sitini
na Saba zilizotumika kwa shughuli za Mishahara pamoja na ununuzi wa vifaa vya
matumizi ya ofisi.
0 Maoni