Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ndugu
Lela Mohammedi Ngozi, wakati akizungumza na wanahabari katika kutoa
kauli ya chama cha Mapinduzi kwa Uongozi wa Mwaka Mmoja Madarakani Rais Hussen Ali Mwinyi
Na Suleiman Kidudu
Chama
mapinduzi CCM Zanzibar kimesema
kinaridhishwa na Kasi ya utendaji kazi wa Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dokta Hussein Ali Mwinyi Ndani ya mwaka Mmoja wa
uongozi wake .
Hayo yameelezwa na
mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm Taifa ndugu Lela Mohammedi Ngozi wakati
Akizungumza na waandishi wa habari Kwa niaba ya Naibu katibu mkuu wa Ccm
Zanzibar Abdlalha Juma Sadala (Mabodi) katika ukumbi wa Afisi Kuu
ya Chama hicho kisiwandui mjini Unguja .
Ndugu Leila emesema
ndani ya mwaka Mmoja tayari ameonesha mwanga wa mafanikio katika sekta mbali
mbali zinazolenga kukuza uchumi wa Nchi pamoja na kukuza uchumi wa Mzanzibar
mmoja mmoja .
Ndugu Lela
amefahamisha kuwa Rais Mwinyi Amedhamiria kuleta mabadiliko ya haraka ndani ya
Zanzibar na kuahidi chama kuendelea kumuunga mkono katika harakati zote za
Maendeleo .
Aidha ndugu Lela
ametaja baadhi ya maeneo ambayo Raisi Mwinyi amefanya kazi ikiwemo kupambana na
wabadhilifu wa Mali za umma ,mapandano dhidi ya udhalilishaji pamoja na
kuendeleza mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwani hayo Yote yamekuwa
yakisababisha ukuaji mdogo wa uchumi wa Taifa .
Katika hatua
nyenginea chama Cha mapundizi kimempongeza Dokta Mwinyi Kwa Kwa kufika
hatua nzuri za ujenzi wa Miradi mikubwa ya kimaendeleo ikiwemo Ujenzi wa
Bandari ya Manga Pwani pamoja na Ujenzi wa Bandari ya Mpiga duri
Katika hatua nyengine
Chama hicho cha Mapinduzi kimempongeza Rais Mwinyi kwakuongeza ukaribu zaid na
Viongozi wa Dini mbali mbali kutokana na umuhimu wao katika Jamii na Mchango
Mkubwa wanaoendelea kuutoa katika Jamii.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa ndugu Lela Mohammedi Ngozi (aliekaa kati kati) kushoto ni Mjumbe wa
Halmashauri kuu Taifa ambae Pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Kichama
Mohamed Rajabu na aliekaa kulia ni Kimtende, Afisa msaidizi katika idara ya
Uenezi Zanzibar
0 Maoni