Na mwandishi wetu
Amesema kwa sasa
kumekithiri vitendo vya uharibifu wa rasilimali za bahari unaofanywa na
binaadamu hali inayopelekea kuharibu mazalia ya samaki hivyo iwapo
taasisi husika zikasimamia sheria hiyo itasaidia kupunguza vitendo hivyo.
Hivyo ameitaka tume ya
sheria kuongeza vifungu vya usimamizi wa samaki wa mapambo na maji baridi ili
kuendana na wakati uliopo.
Nae Afisa kutokea tume
ya kurekebisha sheria Mohammed Abdurahman Mohammed amesema kazi ya ukusanyaji
wa maoni ya sheria namba 7 ya maendeleo ya uvuvi na uhifadhi wa maeneo ya
baharini kwa unguja na pemba imeenda vizuri
Aidha amewataka
wananchi mbalimbali ambao hawajatoa michango yao katika vikao vya ukusanyaji wa
maoni kutumia njia ya maandishi kwa ajili ya kutoa maoni yao na kupeleka katika
idara husika ili kushiriki kwa ajili ya maendeleo ya taifa .
Akifunga kikao
hicho Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya uvuvi na mazao ya baharini Zanzibar
Dk Salum Soud Hammed ameahidi kuzipatia ufumbuzi baadhi ya changamoto ikiwemo
changamoto za leseni kwa wavuvi wa zanzibar na tanzania bara ili kuonesha
kifungu kitachosimamia uvuvi bila ya uonevu kwa pande zote mbili.
Taasisi zilizoshiriki
kikao hicho ni tume ya kurekebisha sheria,idara ya maendeleo ya uvuvi na mazao
baharini na vyombo vya usalama wa raia pamoja na mamlaka za serikali ya
mapinduzi ya zanzibar.




0 Maoni