wanafunzi wa kozi ya Ukocha kisiwani Pemba, wakifuatilia mafunzo ya kozi  hiyo yaliyotolewa na Mkufunzi wa Makocha Muhamed Tajdin

Na Mwandishi wetu Kaije Salum 

Walimu wa mpira wa miguu Visiwani Zanzibar wametakiwa kubadilika kulingana na mabadiliko yanayojitokeza katika soka ili kwenda sambamba na Mabadiliko ya sheria

Kauli hiyo imetolewa na mkufunzi wa makocha Muhamed Tajdin katika Uwanja wa  Gombani Wilaya ya  Chakechake Kisiwani Pemba wakati akiongoza mafunzao kwa wanafunzi wapya wa fani hiyo.

Amesema masomo hayo yatakuwa ya siku kumi na yatahusisha sehemu nne kwa makocha hao wapya ambazo ni kujifunza Nadharia ya mpira, mpira kwa vitendo, tiba na sheria.

Ameeleza sasa niwakati muafaka wa kujenga mahusiano kati ya ZFF na TFF kwa ajili ya kuendeleza na kukuza  soka la Tanzania ambalo limeonesha mwanga wa kupiga hatua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufundi kutoka ZFF Muhamed Said Abdalla alisema kazi ya ukocha ni ngumu na inahitaji kuwa na elimu.

“Awali kulikuwa hakuna vigezo vinavyo hitajika kufundisha lakini sasa wakati umefika kufanya kazi kwa kutumia vielelezo vya kielimu”alisema mkurugenzi huyo.