Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk.Abdulla Sleiman Ali, akipokea boksi la
Vifaa tiba, vitakavyotumika kwa ajili ya upasuaji wa Ngiri katika Hospitali ya
kivunge Unguja na Chakechake kwa upande wa Pemba vifaa hivyo ni msaada kutoka
Serikali ya watu wa China.Na mwandishi wetu
Wizara ya Afya, Ustawi
wa Jamii, Wazee, Jinsia , na Watoto, imepokea msaada wa vifaa vya upasuaji wa
ugonjwa wa Ngiri, vitakavyotumika katika Hospitali ya Kivunge na Chake chake
Pemba.
Akizungumza (kwa njia
ya mtandao) katika halfa ya kukabidhi vifaa hivyo Wizarani hapo, Balozi wa
China aliopo Zanzibar, Zhang Zhisheng amesema msaada huo wa vifaa tiba,
umetolewa kwa lengo la kuwatibu wananchi wenye tatizo la Ngiri.
Ameeleza kuwa,
wagonjwa wasiopungua mia moja (100) watanufaika na msaada huo ili kuimarisha
afya zao, na kuhakikisha tatizo hilo linaondoka nchini.
Balozi Zhang, amesema
Serikali ya watu wa China inaendelea kuisaidia Zanzibar, hasa katika sekta ya
afya na kuahidi kuendeleza ushirikiano ili kuisaidia serikali katika kuimarisha
afya za wananchi wote.
Akizungumza kwa Niaba
ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto, Mkurugenzi Mkuu
wa Wizara hiyo, Dk. Abdulla Suleiman Ali, amesema msaada huo utaweza kuwasaidia
wagonjwa wasiopungua mia nne, jambo ambalo litapelekea kufikia malengo ya Serikali
ya kutoa huduma bora kwa jamii.
Alisema kuwa, misaada
mingi inayotolewa na serikali ya China ikiwemo timu za madaktari, vifaa tiba
pamoja na dawa ni jambo adimu ambalo lina umuhimu mkubwa katika
kuendeleza na kuimarisha huduma za afya nchini.
Aidha Dk. Abdulla
aliupongeza Ubalozi wa china kwa msaada huo na kuahidi kuendeleza ushirikiano
baina ya China na Zanzibar kwa maendeleo ya sekta ya afya




0 Maoni