Waziri Jafo : ujenzi wa Miradi mikubwa uzingatie uhifadhi wa mazingira
SK NEWS
September 01, 2021
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamuwa Rais (Muungano na Mazingira),
Mhe.Selemani Jafo ameelekeza mkandarasi anayetekeza ujenzi wa mradi wa Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) Iyumbu jijini Dodoma kujenga mfumo wa uvunaji maji ili
yasitiririke na kusababisha athari za kimazingira katika Mji wa Dodoma.
Jafo ametoa maelekezo hayo leo Septemba mosi, 2021
alipofanya ziara ya kikazi katika mradi huo wa ujenzi ya kukagua uzingatiaji wa
Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.
Hata hivyo, alionesha kutoridhishwa na kukosekana
kwa mifumo ya uvunaji maji na kuelekeza uongozi unaosimamia mradi kushirikana
na mamlaka zinazohusika na masuala ya usimamizi wa maji kuhakikisha wanajenga
mifumo hiyo.
“Hapa sioni mifumo ya uvunaji wa mvua haya mabati
yatamwaga maji mengi na kusababisha mafuriko leo hii kule Nkuhungu nyumba
zimezama kwa mafuriko, soko la Ndugai na stendi ya Dodoma na maeneo mengine
yatajaa maji sasa tukiwe system ya uvunaji maji tutapunguza mafuriko na pili
tutafanya management (usimamizi) ya maji,” alisema.
Pamoja na hayo pia alizitaka mamlaka zinazohusika na
utoaji wa vibali vya ujenzo kuhakisisha vibali hivyo vinawataka waombaji
kujenga mifumo ya uvunaji maji katika miradi hiyo ili kuzuia maji yasitiririke
ovyo na kusababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo ya miji.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo katika ziara hiyo
iliyolenga kukagua uzingatiaji wa uhifadhi wa mazingira alitoa maelekezo kwa
wakandasi kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo ya miradi wanayojenga.
Alisisitiza kuwa kuwa agenda ya mazingira iwe
kipaumbele cha kwanza katika miradi mikubwa inayotekelezwa nchini na kwamba
wakati wa maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo, eneo hilo lilifyekwa miti
hivyo kuna ulazima wa kupanda miti kwa wingi ili kuliweka katika mazingira
mazuri.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir
Shekimweri alisema pamoja na mradi huo wa nyumba kuwa ni mzuri lakini una
changamoto mbalimbali.
Alisema miongoni mwa changamoto hizo ni kutokufuatwa
kwa masharti yamkataba wa ujenzi ambao ni kumtaka mkandarasi pamoja na mshauri
kufanya kazi bega kwa bega na wadau kama Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Dodoma (DUWASA) ili kupata ushauri usimamizi wa maji.
Naye Mkurugenzi wa Ujenzi wa NHC, Bw. Haikameni
Mlekio amesema wameyapokea maelekezo ya Waziri Jafo na kuahidi Uongozi wa
Shirika hilo utayafanyia kazi. Katika ziara hiyo Waziri Jafo aliambatana na
Meneja wa Baraza la Taifa la
Tags:
Kuhusu SK
Naitwa Suleiman Kidudu, kwa Kifupi "SK", Kitaaluma Mimi ni Mtangazaji na Mwandishi wa Habari, najishughulisha katika kuandaa na Kutangaza Vipindi mbalimbali kuanzia Ngazi ya Habari, Siasa, Michezo, Burudani na Vipindi vya Mapenzi na Mahusiano. Kadhalika nimejikita katika Uandishi wa Habari na Makala za Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi, Burudani na Uandishi wa Simulizi za Mahusiano ya Kimapenzi.





0 Maoni