Na mwandishi wetu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe dkt Hossein Ali Mwinyi amewatoa hofu wananchi walioharibiwa vipando na nyumba zao kupisha ujenzi wa Barabra ya Wete -Gando na Wete- Konde kwamba serikali inajiandaa kuwalipwa fidia zao .
Akizungumza baada ya kupokea malalamiko ya wananchi wakati wa ziara yake kisiwani Pemba , Rais Dk Mwinyi ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na wizara ya Ujenzi , Usafirishaji na Uchukuzi kufanya tathmini upya ili kupata thamani halisi ya fidia kulingana na gharama za wakati uliopo.
Awali Mwakilishi wa Jimbo Mhe Mariam Thani Juma amesema tathimini iliyofanywa imeonyesha kuwepo na baadhi ya wananchi waliovunjiwa nyumba zao kwamba watalipwa shilingi laki moja fadha ambayo haiwezi kukidhi uwezo wa mwanach huyo kujenga nyumba ya kuishi .
Naye Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Salum Mussa Omar amesema moja ya changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo ni suala la kulipwa fidia.
Baadhi ya wananchi wamesema bado wapo baadhi yao hawalipa fidia licha ya kufanyiwa tathmini.





0 Maoni