Mwalikilishi wa jimbo la Mtoni Hussein Ibrahim Makungu (bhaa) amewataka wajumbe wa kamati ya maendeleo ya mfuko wa mwakilishi kuwa wawazi na wakweli ili kuondosha malalamiko kwa wananchi wao.

 Amesema uwazi unatia moyo zaidi kwa wananchi na kujuwa hatuwa zinazochukuliwa na Serikali katika kuwatatulia matatizo yao.

 Akifunguwa kikao cha kamati ya maendeleo ya mfuko wa maendeleo ya mwakilishi huko katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar ocean view kilimani Amesema pesa za mfuko wa maendeleo ya mwakilishi ni fedha za wananchi hivyo Ni vyema kuwaachia kuweka vipao mbele wanavyohitaji katika maeneo yao.

 Aidha amewataka kuweka kumbukumbu na vielelezo sahihi ili kuweza kuwasaidia katika kuweka hesabu vizuri wakati wa ukaguzi.

 Hata hivyo amewataka kutumia mfumo wa pesa kwa thamani ili kuondosha ubabaishaji unaoweza kujitokeza.

 Kwa upande wake katibu wa kamati ya maendeleo ya mfuko wa mwakilishi wa Jimbo la mtoni Maryam suleimani Bakari amesema kikao hicho kimeweza kusaidia kuibuwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao na kupata fursa ya wajumbe hao kutoa mapendekezo na kufanyiwa kazi kwa haraka.

 Nao wajumbe wa kamati hiyo Wameahidi kuzitumia sh.milioni 20 za mfuko wa maendeleo ya mwakilishi kwa mujibu wa vipao mbele walivyokubaliana na kuwaomba wananchi kuwaunga ili  kufifikia malengo yaliokusudiwa.

 Wajumbe wa kamati ya mfuko wa maendeleo ya mwakilishi wa Jimbo la mtoni wameweka vipao mbele katika sekta ya maji, umeme, njia za ndani na vikundi vya ushirika ili kuondosha usumbufu wanaoupata wananchi wao.