Mwakilishi wa Jimbo la mpendae shaaban Ali othman  wa pili kutoka kushoto, akizungumza na Wajumbe wa mkutano wa halmashauri ya ccm wadi ya mpendae.

Na Mwandishi wetu

Mwakilishi wa Jimbo la mpendae shaaban Ali othman Amewataka Wanachama wa chama cha mapinduzi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufànyika mwaka 2022  ili waweze  kuchaguwa viongozi Bora na makini.

 Ameyasema hayo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mpendae Mkoa wa Mjini wakati akifungua mkutano wa halmashauri ya ccm wadi ya mpendae.

 Amewasihi wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuendelea kushirikiana kwa kuchaguwa viongozi watakaoendelea kupeleka mbele jahazi la chama hicho kikonge hapa nchini.

 Aidha Amewataka wanaCCM wakati wa Uchaguzi wa Chama ukifika wajitahidi  kuchagua viongozi ambao watakuwa hawana ubaguzi,fitna majungu na kuwaletea maendeleo ya haraka.

 Hata hivyo ameahidi kuwa viongozi wa Jimbo hilo watasimamia kwa nguvu zote kwa kuhakikisha hakuna mtu atakaeharibu uchaguzi katika Jimbo Hilo.

 Kwa upande wake katibu wa chama Cha mapinduzi wadi ya mpendae Tasiana Antony Roman Amesema uhai wa chama Ni vikao hivyo Ni vyema kufanya vikao kama inavyotakiwa ili wapate kujuwa Mambo muhimu katika kuendesha chama na Jumuiya zake.

 Katika mkutano huo kumewasilishwa ripoti mablimbali ikiwemo Uongozi,utekelezaji wa ilani, ripoti ya chama kwa kipindi Cha miezi 6, Hali ya siasa, uchumi na maendeleo katika wadi ya Mpendae.

wajumbe wa mkutano wa halmashauri ya ccm wadi ya mpendae wakishiriki katika mkutano wa Wadi hiyo