Makamu
wa Kwanza wa rais wa Zanzibar Mhe. Othman Msoud Oudhman, amesema Zanzibar na
Oman zinaweza kutumia historia na uhusiano wa damu uliopo wa muda ili kuibua
fursa mpya zaidi za uwekezaji ili
kusaidia kukuza uchumi na maendeleo ya kijamii.
Mhe.
Othman ameyasema hayo leo Ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar, alipozungunza
na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi.
Aidha
amefafanua kwamba yapo maeneo mengi ambayo kimsingi, yanaweza kujadiliwa
zaidi na baadae kujengewa ushirikiano unaoweza kusaidia manufaa kwa Zanzibar na
Oman.
Mhe Othman amemueleza Balozi Al Sinawi kwamba Suala la mahkama ya Kadhi, fursa za masomo
na kubadilishana uzoefu ni miongoni mwa maeneo muhimu, ambayo serikali hizo
mbili zinaweza kujadiliana na kukubaliana kuongezwa ushirikiano kwa kuwa yana
mchango mkubwa katika historia Oman na Zanzibar.
Amesema kwamba Oman inazoefu mkubwa katika kusimamia mahkama za kadhi na kwa vile ni waazilishi wa mahakama hiyo hapa Zanzibar ni muhimu kuongeza ushirikiano katika kusaidia mbinu za uendeshaji na usimamizi wa hakama hizo Zanzibar.
Pia
Mhe. Othman alimweleza Balozi huyo kwamba hivi sasa Zanzibar inatekeleza sera
yake ya Uchumi wa Bluu, na imeweka
mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya
kuendeleza uwekezaji na kusaidia nchi kukuza uchumi.
Naye Balozi Al Sinawi alimueleza Mhe. Makamu kwamba , Oman ipo tayari kuendeleza ushirikiano wa historia uliopo katika sekta mbali mbali na kwamba anaichukulia Zanzibar kuwa ni nyumbani kutokana udugu wa damu uliopo kwa muda mrefu.
Aidha
amesema kwamba serikali ya Oman ina nia thabiti ya kusaidia Zanzibar na
Tanzania kwa jumla katika maeneo mabali mbali, licha kwamba maradhi ya UVIKO 19
imekuwa ni kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa mambo mbali mbali hivi sasa.
Pia
Mhe. Sinawi amesema kwamba nchi yake na Zanzibar tayari inayomakubaliano ya
ushirikiano katika kuendeleza sekta ya biashara
utalii ambayo inasaidia sana kukuza uchumi na maeneleo.





0 Maoni