Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Pemba Asya Sharif Omari amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kuhudhuria Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, uliofanyika jana September 21,Nchini Marekani.

Mhe Asya amesema kitendo cha Rais Samia kusafiri hadi Nchini Marekani kwaajili ya kuhudhuria mkutano huo ni jambo jema kwakua Tanzania ni sehemu ya Dunia hivyo inahitaji kushirikiana na Mataifa Mengine Dunia katika kila Jambo hasa ukiangalia umuhimu wa Mkutano wenyewe.

‘‘Rais samia anafanya kazi kubwa sana, tumeona tokea aapishwe amekua akifanya kazi kubwa ndani na Nje ya nchi , lakini kubwa amekua akizunguka kuangalia namna gani atashirikiana na mataifa mengine kwaajili ya maendeleo ya Tanzania,  kwakweli anatuwakilisha vizuri na anaionesha Dunia kuwa Wanawake tunaweza’’amesema Mh Asya.

Mhe Asya amesema hayo leo (September 22) akiwa Visiwani Zanzibar wakati wa mazungumzo na mwandishi wetu ambapo amesema safari hizo za Mhe Samia zina umuhimu mkubwa na hasa ukizingatia kipindi hichi cha korona kila taifa linaangalia namna gani ya kusimama kwaajili ya kuboresha uchumi wake uliotetereka kwa Uvico 19.

Katika hatua nyengine Mhe Asya amesema Rais Samia anafanya kazi kubwa ya kuitangaza Tanzania Kimataifa hivyo watanzania watarajie kuendelea kuona maendeleo mengine makubwa ikiwemo kuongezeka kwa wawekezaji na kuimarika kwa diplomasia zaidi katika kipindi hiki cha uongozi wake.

‘‘unajua ndugu mwandishi juzi tu tumeshuhudia Rais akirekodi kipindi maalum cha Royal Tour,  kile kipindi kitakwenda kuitangaza Tanzania na sasa tutarajie kuona watalii wengi  wakiingia Tanzania na Zanzibar na hata wawekezaji lakini kubwa kuimarika kwa Diplomasia kati ya mataifa ya Nje na Tanzania’’ amesema Mhe Asya

Rais Samia ni Miongoni mwa Viongozi wakuu wa Nchi waliohudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa 76 uliofanyika  Nchini Marekani.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia leo pia amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Comoro, Mhe. Azali Asoumani na Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, Mhe. Rebecca Nyandeng Garang. Viongozi hao wamezungumzia kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na mataifa hayo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Comoro Mhe. Azali Assouman, walipokutana Jijini New York Nchini Marekani jana Sept 20,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Mhe. Rebbeca Nyandeng Garang, walipokutana Jijini New York Nchini Marekani jana Sept 21,2021.