Na mwandishi wetu
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar
itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Oman kwa maslahi ya wanachi wake
baina ya pande mbili.
Mhe. Hemed ameleza
hayo Afisini kwake Vuga alipokutana na Balozi Mdogo wa Oman SAID ALSINAWI
alipofika kwa ajili ya kujitambulisha.
Amesema Serkali ya
Mapinduzi Zanzibar inathamini ushirikiano wa kihistoria uliokuwepo kwa muda
mrefu ambapo Oman imekuwa ikiunga mkongo Zanzibar kupitia sekta mbali mbali
ikiwemo kuimarisha elimu kwa wananchi wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais
alimueleza Balozi huyo wa Oman anaefanyia kazi zake Zanzibar kuwa, Wakati
umefika kwa nchi hiyo kuja kuekeza Zanzibar ikizingatiwa kwa sasa Zanzibar
imejikita kukuza uchumi wa ke kupitia sekta ya Uchumi wa Buluu (Blue Economy).
Katika mazungumzo yao,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishia Balozi SAID ALSINAWI
kumpatia ushirikiano wa karibu wakati akitekeleza majukumu yake hap Zanzibar.
Nae, Balozi mdogo wa
Oman SAID ALSINAWI alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nchi ya Oman
itaendelea kushirikiana na Zanzibar kutokana na uhusiano wake wa kidugu wa
miaka mingi iliopita.
Kuhusu suala zima la
Uwekezaji, Balozi SAID ALSINAWI alisema Oman tayari imeonesha nia yake ya
kuekeza Zanzibar kupitia sekta mbali mbali ambapo kwa sasa mipango hiyo
ipo katika machakato.
Alieleza kwamba, Ujio
wa Ndege yao ya Oman Air ikiwa imebeba abiria wa kutosha kwa safari zake hapa
Zanzibar ni kielelezo tosha cha ushirikiano baina ya nchi mbili hizo.





0 Maoni