Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (wa pili kuli) akiwa kwenye picha ya pamoja na na
Waziri wa Utalii wa Zimbabwe mara baada ya kikao cha kujadili
uwindaji wa kitalii pembeni mwa Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa
Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini
Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni
kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.Kulia ni
Balozi wa Paris Ufaransa Mhe.Samweli Shekindo pamoja Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii ya Zimbabwe Dnomal dinamo Na mwandishi wetu
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amezitaka nchi za Afrika kuwa na kauli moja kuhusu
taratibu na bei za wanyamapori katika biashara za uwindaji wa
kiutalii
Ametoa kauli hiyo
alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao vyz ana kwa
ana na baadhi ya mawaziri wa Utalii wa nchi za Afrika katika Mkutano wa
64 wa Kimataifa wa Utalii uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la
Utalii Duniani (INWTO) unaofanyika kwa muda wa siku nne nchini Cape
Verde.
Amesema bei za wanyama
wanaoruhusiwa kuwindwa pamoja na vitalu vya uwindaji wa Wanyamapori zimekuwa
zikitofautiana sana kati ya nchi na hali hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa
shughuli uhifadhi barani Afrika.
Akizungumza katika
vikao hivyo vya ana kwa ana na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe.Mhe.Ngobhithize
Ndlovu amezitaka nchi hizo kuwa kitu kimoja katika kuamua na kupanga bei
za uwindaji wa Kitalii.
Amesema kutokana na
kutofautiana kwa bei na baadhi ya kanuni na taratibu hizo Wawindaji
wa kiitalii wamekuwa wakitumia mwanya huo kuzikandamiza nchi za Kiafrika
kwa kupanga bei wanazotaka wao huku wakidai kuwa bei hizo cha chini zimekuwa
katika nchi nyingine pia.
Amesema Wawindaji hao
wamekuwa wakipanga bei za uwindaji wa kiutalii na sio nchi husika huku
wakidai kuwa kama bei hiyo haitawezekana basi watakwenda katika nchi nyingine
ambayo utalii wake uwindaji ni bei ya chini zaidi
" Utofauti wetu
huu umekuwa ukitukandamiza kama nchi kwani tulitakiwa sisi ndo tupange bei
lakini kutokana na kutokuwa na umoja bei za wanyama zimekuwa zimekuwa
zikiamuliwa na wao hili lazima tulikatae kwa kuungana kwa pamoja "
alisisitiza Dkt.Ndumbaro
Kufuatia hali hiyo,
Dkt.Ndumbaro amezitaka nchi zote zinazoendesha utalii wa uwindaji zifanye
mkutano kwa nji ya mtandao ili kujadili mustakabali wa biashara hiyo na
kisha zitoke na kauli moja ili kuwathibiti wawindaji wa kitalii kwa ajili
ya maslahi mapana ya uhifadhi barani Afrika.
Amezitaja baadhi ya
nchi wanachama wa SADC zinazofanya vizuri katika uwindaji wa kitalii kuwa ni
Botswana, Zimbabwe pamoja, Zambia na Afrika ya Kusini
Katika hatua nyingine
, Dkt.Ndumbaro ametoa ahadi kwa nchi ya Zimbabwe kama itakuwa
tayari ipewe mafunzo ya kuendesha biashara ya uwindaji wa kiutalii kwa mfumo wa
kidigitali ambao utasaidia kuongeza mapato maradufu
Amesema tangu
kuanzisha kwa mfumo huo nchini Tanzania umeleta manufaa makubwa kwa nchi
ambapo Wawindaji wa kitalii ili kuweza kupata vitalu vya uwindaji wamekuwa
wakilazika kushiriki katika mnada wa kimtandao.
Naye, Waziri waUtalii
wa ZimbabweMhe.Ngobhitithize Ndlovu amesema nchi za kiafrika lazima ziungane
katika suala hilo kwani katika nchi ya Zimbabwe Wawindaji hao pia wamekuwa
wakipanga bei huku wakidai kama hiyo bei haitawezekana watakwenda Tanzania
ambako bei vitalu vya uwindaji ipo chini zaidi
Amesisitiza kuwa
shughuli za uhifadhi zimekuwa aghali sana huku biashara hiyo ya uwindaji wa
kiutalii ukibaki pale pale kutokana na kutofautiana kutoka nchi moja hadi
nyingine
Naye, Kamishna
Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi
amesema umoja huo wa nchi za Kiafrika katika biashara ya vitalu vya uwindaji
italiingizia taifa fedha nyingi za kigeni sio kwa Tanzania pekee bali kwa
Afrika nzima
" Biashara hiyo
imekuwa na ushindani baina yetu bila kujuana kufuatia kila nchi kupanga bei
zake kulingana na matakwa ya wadau hao huku shughuli za uhifadhi zikiwa juu
zaidi" amesisitiza Kamishna Mabula.
0 Maoni