Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akieleeza umuhimu wa vyombo vya habari kuwaunga mkono wanake kushika nafasi za uongozi.

 Mkurugenzi wa Chama cha Waaandishi wa habari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema katika jitihada za kuwaunga mkono wanawake kushika nafasi mbali mbali za uongozi vyombo vya habari vinawajibu wa kutoa kipao mbele habari zinazowahusu wanawake viongozi na wale wote ambao wanahitaji kupaziwa sauti zao kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii.

 Dkt,Mzuri ameyasema hayo huko Tunguu Wilaya ya kati Unguja katika ofisi za Chama hicho kufuatia uzinduzi wa ripoti ndogo ambayo inatazama kwanamna gani vyombo vya habri vinawaandika ama kuwaripoti wanawake viongozi katika habari za kila siku visiwani hapa.

 Amesema  kwa kuwa vyombo vya habari vinanafasi kubwa ya kufanya mabadiliko wakati huu ikiwa ni kuandika na kuripoti matukio mbali mbali yanayofanywa na wanawake viongozi Serikali n ahata wasiokua viongozi ndani ya Serikali.

 Amesema vyombo vya habari kupitia mkakati maalumu wanawake kuwaandaa  wanawake kushika nafasi za uongozi kupitia vipindi vyao vya kila siku kwani wanawake ni watu wanaoitaji motisha.

 Ameeleza kuwa kikawaida wanawake wengi wamekua wakishindwa kusika nafasi za uongozi kutokana na kukosa maandalizi bora ya kutaka kushika nafasi hizo badala yake wengi wao huamua kujitokeza kugombea nafasi hizo bila kukosa maandalizi mazuri ya awali.

 Akiendelea kufafanua zaidi Mkurugenzi huyo alimtolea mfano Rais Samia Suluhu na kueleza kuwa ni mtu aliepitia hatia hatua mbali mbali hadi kufika kuwa Rais na niwazi kwamba ni miongoni mwa wanawake walioandaliwa na kujitengeneza vyema kushika nafasi tofauti mpaka kuwa Raisi.

 Akiwasilisha ripoti hio mkufunzi wa maswala ya habari Dkt,Abuubakar Rajab alisema  kupitia utafiti wake wa vyombo mbali mbali vya habari vinavyofanya kazi visiwani hapa na Tanzania kwa ujumla bado vimekua vikitoa nafasi ndogo sana kwa viongozi wanawake.

 Amesema imekua kawaida kutoona habari ianyomuhusu mwanamke kupewa kipao mbele kwenye magazeti au ata redio badala yake wengi wao wanaamini kuwa wanaume ndio wanaopaswa kupewa kipao mbele kila leo.

 Kwa upande wake mratibu wa mradi wa ushirikishwaji  wanawake katika  uongozi kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi alisema mradi huo wa miaka mine unalenga kuwawezesha wanawake elfu sita kutoka wilaya 11 za Unguja na Pemba.

 Amesema anaamini elimu watakayopatiwa wanufaika wa mradi huo italeta tija hatimae wanawake wengi wataweza kushika nafasi mbali mbali za uongozi iwe kwenye jamii zao au hata za kisiasa.

 Mradi wa ushirikishwaji  wanawake katika nafasi za uongozi unatekelezwa na TAMWA-ZNZ chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.

 

Mratib wa mradi wa ushirikishwaji wanawake kushika nafasi za uongozi Salma Amiri Lusangi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.

Mkufunzi wa maswala ya habari Zanzibar Dkt,Abuubakari Rajab akiwasilisha ripoti juu ya uwakilishi wa habari za wanawake katika vyombo mbali mbali.
Mwandishi wa habari wa gazeti habari leo upande wa Zanzibar Khatin Suleiman akichangia ripoti hio mara baada ya kuwasilishwa.