Mkurugenzi wa
TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akizungumza kuhusu umuhimu wa wanawahabari kujikita na
kupaza sauti za wanawake ili waweze kushiriki katika nafasi za uongozi na
demokrasia.Na mwandishi wetu
Mkurugenzi wa Chama
cha waandishi wa habari TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema ushiriki wa wanawake
katika nafasi mbali mbali za uongozi wa kisiasa na kijamii huchangia kwa kiasi
kikubwa maendeleo ya jamii za na Nchi kwa ujumla, kwani wanawake ni watu weye uwezo
mkubwa na wepesi wa kutekeleza majukumu yao.
Dkt,Mzuri aliyasema hayo wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku 3 ya waandishi wa habari 30 wa vyombo mbali mbali Zanzibar kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na demokrasia.
Alieleza kuwa Taifa lolote lile haliwezi kupiga hatua za kimaendeleo zaidi iwapo litawaacha wanawake nyuma na kuendeleza imani yakuwa wanawake hawapaswi kuwa viongozi katika nyanja za kitaifa na hata kijamii.
Katika hatua nyengine alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya wanajamii kuendelea kuamini kuwa kushiriki kwa wanawake kwenye uongozi ni chanzo kikubwa cha uhuni huku wakisahau pia uhuni huo unaweza kufanywa hata na wanaume wanapokua kiongozi lakini kwa makusudi ya kuwachafua wanawake jamii imebeba taaswira hio potofu.




0 Maoni