Watendaji wa shirika la umeme Zanzibar Zeco wakitekeleza wajibu wao wakuboresha miundombinu ya umeme katika moja ya maeneo visiwani Zanzibar
 

Na mwandishi wetu

Shirika la Umeme Zanzibar ZECO limewataka wananchi kuacha tabia ya kuaharibu miundombinu ya umeme katika maeneo yao kwakua kufanya hivyo kunasababisha hasara kwa shirika na Jamii kwa ujumla.

 Amesema kumekua na tabia za baadhi ya watu wasiokuwa wazalendo nan chi yao wamekua wakikata waya za transfoma na kusababisha kukosekana kwa  huduma ya Umeme katika laini zao au kuengeneza shoti inayokwenda kuharibu vitu vya wananchi.

 Meneja mawasiliano na huduma kwa wateja wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO Salum Abdalla Hassan amesema hayo kufuatia kuwepo kwa baadhi ya wananchi kuwa na tabia ya kukata waya katika transfoma na kwenda kuziuza hali inayopelekea kukosa ulizi wa kudhibiti radi pindi zinapopiga katika tranfoma na kupelekea tranfoma kuungua.

 Amesema serikali inatumia pesa nyingi kwa ajili kufikisha miundombinu ya Umeme kwa wananchi wake lakini kunawatu kwa makusudi wanaifanyia uharibifu na kupelekea kukosekana kwa  huduma ya umeme.

 Katika hatua nyengine  Salum amewaomba wananchi kuilinda miundombinu iliyokuwepo karibu na makaazi yao ili isifanyiwe hujuma  kwani iwapo kifaa kidogo kikafanyiwa hujuma katika tranfoma kinaweza kuleta athari kubwa