Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Fedha na mipango Zanzibar, Jamal Kassim amesema Zanzibar imepata mgao wa sh. Milioni 971, laki nne, 69 elfu, 652 kutokana na makusanyo ya tozo ya miamala ya simu kati ya Julai 15 hadi 31 Mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wetu Ofisini kwake Vuga Mjini Unguja mhe. Jamal Kassim amesema mgao huo wa fedha
unatokana na makusanyo ya jumla sh. bilioni 23.6 katika kipindi hicho cha wiki
mbili zilizokusanywa Zanzbar.
Ameeleza fedha zilizozipata Zanzibar umeekwa kwenye
mfuko maalumu kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara za
ndani kwa kiwango cha lami.
Mhe. Jamal amesema kuna muongozo maalumu unaosimamia
namna ya kukokotoa fedha zinazokusanywa ili kupata mgao wa fedha hizo za
makusanyo ya tozo kwa upande wa Zanzibar.
Aidha amewasihi wananchi kuendelea kutumia huduma za
miamala ya simu ili kuchangia shughuli za maendeleo katika Taifa.





0 Maoni