Timu ya Yanga imewapiku mahasimu wao Simba baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya kiungo wa Kimataifa Raia wa Uganda Halid Aucho

Aucho alitua hapa Nchini hivi karibuni kwaajili ya kuja kuzungumza na Viongozi wa Simba baada ya kumpa Mualiko hata hivyo inaonekana Dili hilo  halikufanikiwa

kwa sasa Aucho yuko kwao Uganda akirejea karibuni kutoka hapa Tanzania baada ya Yanga kupindua Meza ya Mahasimu wao na kumalizana na Mchezaji hyo

Dili la Aucho kwa Simba huenda lilikwama kwa kile kilichoelezwa kuwa Jamaa alihitaji kiwango kikubwa cha Mshahara jambo ambalo Yanga walifikia Makubaliano na Kumalizana nae

Akiwa kwao Uganda, Aucho amethibitisha ni kweli alikuwa Tanzania lakini hakutaka kuweka wazi ni timu ipi amemalizana nayo akisema klabu ndio yenye jukumu la kutangaza usajili wake, ingawa habari za ndani zinaeleza kuwa Yanga tayari wameshamalizana nae.