Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Dkt. Saada Mkuya Salum akimvisha Medali  mshindi wa tatu katika mbio za mita 100 za ulemavu wa usikivu Murtala issa Daudi katika Bonaza la shamra shamra za kuelekea siku ya Vijana Duniani hafla iliyofanyika Uwanja wa Amani .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Dkt. Saada Mkuya, amesema atahakikisha haki za watu wenye ulemavu zinashughulikiwa katika nyanja zote za maendeleo.

Akizungumza katika bonaza la shamra shamra za kuelekea siku ya Vijana Duniani, lililofanyika Uwanja wa Amani Mjini Unguja, amesema watu wenye ulemavu wanauwezo mkubwa wa kichumi na kiakili hivyo ipo haja ya kupewa kipaombele.

Ameeleza kuwa, watu wenye ulemavu wanauwezo wa kufanya shughuli mbali mbali za kijamii ambazo zinaweza kuwainua kiuchumi ikiwemo michezo hivyo ni muhimu kupewa haki zao.

Aidha Dkt. Saada amesema watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa wa kushiriki michezo mbali mbali kama wanavyoshiriki watu wengine hivyo ni vyema yanapofanywa mabonaza washirikishwe ili waoneshe uwezo wao.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya Madrasa Early Childhood, Sharifa Suleiman amesema wameamua kuzielekeza jitihada zao kwenye bonaza hilo, kwani wanaamini michezo ina manufaa makubwa katika kukuza afya ya mwili, akili, kijinsia na kijamii.

Mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu Mwandawa Khamis amesema bonaza hilo limethibitisha wazi kuwa watu wenye ulemavu wanauwezo  wa kushiriki katika  michezo mbalimbali kama binadamu wa kawaida.

Bonaza hilo lenye Kaulimbiu “michezo na lishe bora kwa afya ya vijana wenye ulemavu” linahusisha michezo mbalimbali ikiwemo, riadha, kuvuta kamba, kufukuza kuku, mpira na mchezo wa mpira kwa watu wasioona.

Mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye Ulemavu Zanzibar  Mwandawa Khamis Mohamed akielezea umuhimu wa watu wenye Ulemavu katika  Bonaza la shamra shamra za kuelekea siku ya Vijana Duniani lililowashirikisha watu hao huko Uwanja wa Amani Zanzibar. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Dk. Saada Mkuya Salum akizungumza na waandaaji na washiriki wa Bonaza la shamra shamra za kuelekea siku ya Vijana Duniani lililowashirikisha watu wenye Ulemavu katika Uwanja wa Amani Mjini Unguja.  


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Dkt. Saada Mkuya Salum akimvisha Medali mshindi wa kwanza katika mbio za mita 100 za Ulemavu wa Viungo Suleiman Hassan katika Bonaza la shamra shamra za kuelekea siku ya Vijana Duniani huko Uwanja wa Amani Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mbio za mita 100 zilizojumuisha watu wenye ulemavu wa Usikivu na Viungo wakikimbia katika mashindano hayo ya Bonaza la shamra shamra za kuelekea siku ya Vijana Duniani yaliyofanyika Uwanja wa