Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa
ameagiza kusimamishwa kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Buza Wilaya ya
Temeke Mkoa wa Dar Es Salam hadi hapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu atakapojiridhisha ni mradi gani
unapaswa kufanyika katika eneo hilo.
Katika taarifa yake hiyo aliyoitoa mbele ya wananchi wa Buza wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua miradi ya kimaendeleo Temeke, amewataka wananchi kuondoa hofu na Uongozi wa Rais Samia kwakua Serikali yake iko makini kuhakikisha Miradi yote nchini inatekelezwa kwa viwango na gharama halisi bila ya kupoteza hata shilingo moja ambayo ni kodi ya wananchi
Katika hatua nyengine, Waziri Mkuu ameitaka TAKUKURU ifanye uchunguzi ili kubaini ni kwanini uongozi wa Manispaa hiyo ulianza kulipa mkopo huo miezi miwili baada ya kuupokea mkopo huo huku mkataba ukionesha kuwa wanaweza kulipa deni hilo baada ya miezi sita kulingana na muda wa matazamio.
PONYEZA LINK HAPO CHINI KUANGALIA VIDEO YA TUKIO LA KUSITISHWA KWA UJENZI WA SOKO





0 Maoni