Waziri wa nchi, ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ, Masoud Ali amewataka watoaji huduma za wakala za kijamii kuacha urasimu katika utoaji wa huduma hizo.
Amewasisitiza watendaji wa taasisi hiyo hususani
wale wa chini kutekeleza vyema majukumu yao vyema, kuwa na majibu mazuri pamoja
na kutoa huduma kwa wakati ili kupunguza msongamano wa wananchi katika ofisi
hiyo.
Aidha amewataka watendaji wa ofisi hiyo ya wakala wa
huduma za Kijamii iliyopo Mazizini, Unguja kuzingatia sheria namba 3 ya mwaka
2018 ya matukio ya kijamii kutambua mfumo na vigezio vya utoaji wa huduma ya
upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa ili kuondoa changamoto ya utoaji wa vyeti
hivyo kwa wale wasio na uhalali.
Sambamba na hayo licha ya kuahidi kutetea maslahi ya
watumishi wa taasisi hiyo amewataka kuacha tabia ya kushirikiana na vishoka
katika utoaji wa vyeti feki kwani hatua hiyo inachochea ongezeko la vyeti feki.
Ameonya kuwa Serikali itachukua hatua kali kwa
mtumishi yeyote atakaebainika kujihusisha na vitendo hivyo.





0 Maoni