Na mwandishi wetu
Waziri wa Afya ,Ustawi wa Jamii, Wazee ,Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui amewataka watendaji wa wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya awamu ya nane.
Hayo ameyasema katika
hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Katibu Mkuu yaliyofanyika Wizarani hapo
mara baada ya kuapishwa kwa Katibu Mkuu mpya waWizara hiyo
Mazrui amewataka
watendaji kujitathmini ili waweze kuimarisha utendaji wa kazi, pamoja na
kurekebisha kasoro zinazojitokeza kwa lengo la kuleta ufanisi kazini.
Akizungumza mara baada
ya kukabidhiwa ofisi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Ustawi wa Jamii, Wazee
,Jinsia na Watoto Dkt Fatma Mrisho amesema atahakikisha kila mwananchi anapata
huduma bora za afya katika maeneo yote ya mijini na vijijini.
Amewataka wafanyakazi
kubuni mikakati itakayosaidia katika kuleta maendeleo ya sekta ya afya.
Waziri wa Afya ,Ustawi wa Jamii, Wazee ,Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na watendaji wa Wizara hiyo kuhusiana na mashirikiano mazuri baina yao na Katibu wa Wizara hiyo aliyeteuliwa hivi karibuni katika hafla ya makabidhiano ya Wizara iliyofanyika Ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Unguja.





0 Maoni